Wimbi la ajali limezidi kujitokeza nchini Tanzania ambapo leo Jumanne May 9, 2017 basi la Ally's Star lenye namba za usajili T402 ATV likisafiri kutoka Mwanza kwenda Kaliua Tabora limegongana uso kwa uso na basi la Isanzu T797 DDW lililokuwa likitoka Kahama kwenda Mwanza.
Ajali hiyo imetokea leo majira ya saa mbili asubuhi katika eneo la Samuye barabara ya Shinyanga kwenda Mwanza.
Inaelezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa basi la Ally's Star aliyekuwa anajaribu kulipita gari aina ya Scania T784 BMT lililokuwa limeharibika pembezoni kwa barabara,ndipo akagongana na basi la Isanzu.

Hakuna mtu aliyepoteza maisha katika ajali hiyo lakini abiria 35 katika magari yote mawili wamejeruhiwa na wamekimbizwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga.