Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) imewakutanisha wadau mbalimbali wa maendeleo nchini kuijadili bajeti ya Tanzania ya mwaka wa fedha 2016/2017 ambao unaelekea kuisha. Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida alisema mdahalo huo ni sehemu ya shughuli ambazo zinafanywa na ESRF ili kutazama ni njinsi gani Taasisi inaweza kuisaidia Serikali kuweka mipango thabiti kwa ajili ya maendeleo ya nchi. Dkt. Kida alisema mdahalo huo ulihusu bajeti ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kuangalia utekelezaji wa bajeti zilizopitishwa kwa mwaka wa fedha 2016/2017, changamoto zilizopo na nini kifanyike katika bajeti ya 2017/2018.
Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida akitoa neno la ufunguzi.
“ESRF imekuwa ikishirikiana na wadau ili kuangalia ni jinsi gani tunaweza kusaidia mchakato wa maendeleo wa nchi yetu kwa njia ya utafiti mbalimbali, uchambuzi na utayarishaji wa sera na kuongeza wadau uwezo kupitia mafunzo mbalimbali.
“Kama jinsi mnavyojua nchi yetu imekuwa na mipango ya maendeleo ambayo inatekelezwa kupitia bajeti kwa kuangalia mambo yenye umuhimu kwa Taifa, bajeti imekuwa ikipangwa kila mwaka kwa kuzingatia maeneo ya kuyapa kipaumbele ili kuleta maendeleo kwa nchi.” alisema Dkt. Kida.
Kwa upande wa mtoa taarifa ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Joviter Katabaro (Mkufunzi katika, shule ya Elimu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam) alisema pamoja na serikali kutoa elimu bure katika ngazi fulani ya elimu nchini lakini bado kuna changamoto mbalimbali katika elimu ambazo zinahitaji kutafutiwa ufumbuzi katika bajeti ya 2017/2018. Mhadhiri Mwandamizi wa Shule Kuu ya Elimu Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Dk. Joviter Katabaro akitoa taarifa kuhusu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
“Pamoja na jitihada kubwa ya Serikali katika elimu bado kuna upungufu wa majengo 10,000 ya shule nchini kitoke, kuna upungufu wa maktaba 15,000, vyoo bado havitoshi,” alisema Dk. Katabaro. Kwa upande wake, Prof. Haidari Amani (Mtafiti Mshirki mwandamizi ESRF) ambaye alitoa taarifa kuhusu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi alisema pamoja na sekta ya kilimo kuwa na changamoto ambazo zinajitokeza serikali inatakiwa iweke mfumo mzuri kuanzia wakulima wadogo ili waweze kunufaika na kilimo ambacho wanakifanya. Mtafiti Mwenza wa ESRF, John Shilinde akitoa taarifa kuhusu Bajeti ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi. Mtafiti Mwenza Kiongozi wa ESRF, Prof. Haidari Amani akijibu maswali ya baadhi ya washiriki waliohudhuria. Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida akifafanua jambo wakati wa kuijadili bajeti ya 2016/2017 katika sekta za Elimu na Kilimo. Picha juu na chini ni baadhi ya washiriki wakitoa maoni na kuuliza maswali kuhusu bajeti zilizotolewa taarifa. Baadhi ya wadau mbalimbali wa maendeleo nchini walioshiriki kuijadili bajeti ya Tanzania ya mwaka wa fedha 2016/2017 katika sekta za Elimu na Kilimo.