Msanii nyota wa filamu Tanzania, ambaye pia ni balozi wa Biko, Kajala Masanja, akionyesha namba ya ushindi wa Sh Milioni 10 aliyoshinda mkazi wa Mwanza, Pildas Emmanuel katika mchezo wa kubahatisha unaoendeshwa na Kampuni ya Biko Tanzania. Droo hiyo ilichezeshwa jana, jijini Dar es Salaam. Picha na Mpiga Picha Wetu.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MKAZI wa Mwanza, Pildas Emmanuel ameibuka na ushindi mnono wa Sh Milioni 10 kutoka kwenye shindano la ‘Ijue Nguvu ya Buku’ katika droo iliyochezeshwa jana jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa pia na msimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abdallah Hemed.
Droo ya bahati nasibu hiyo inayoendeshwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi katika simu za mikononi kupitia huduma za Tigo Pesa, Airtel Money na M-Pesa ambapo pia ilichezeshwa na Balozi wa Biko Tanzania, Kajala Masanja.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Biko Tanzania, Charles Mgeta, alisema kwamba droo hiyo imeshirikisha washiriki zaidi ya 10,000 Tanzania nzima na kufanikiwa Emmanuel kutoka Mwanza kunyakua fedha hizo na kuingia katika historia ya mshindi wa kwanza kutoka mkoani.
Alisema Biko wamefurahia kuona mshindi wa droo ya tatu ametoka mkoani, baada ya droo mbili za awali ambazo zote washindi wake walitoka jijini Dar es Salaam kwa Christopher Mgaya na Nichoulas Mlasu kuibuka na Milioni 10.
“Tunawapongeza washiriki wote wanaogombania gurudumu la mchezo wetu wa Biko ambao umeshika kasi, huku nikimpongeza pia mshindi wetu wa mkoani Mwanza, Emmanuel kuibuka na ushindi huu ambao kwa hakika unaweza kubadilisha maisha yake.
“Bado kila mtu anaweza kuibuka na ushindi wa Sh Milioni 10 kwa droo ya wiki pamoja na zawadi za papo kwa papo kuanzia Sh 5000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000 500,000 na Milioni moja kwa kucheza Biko mara nyingi zaidi kwa kufanya miamala kwenye simu zao za mikononi huku namba yetu ya kampuni ikiwa ni 505050 na namba ya kumbukumbu ni 2456,” Alisema.
Naye Emmanuel alisema bado haamini ametangazwa kushinda zawadi hiyo inayoweza kumfanya atimiz ndoto zake za kimaisha kwa kuhakikisha kwamba fedha hizo anazitumia vizuri endapo atakabidhiwa kutoka Biko, huku akikiri kuwa ametokea kuupenda mchezo wa Biko.
“Nimekuwa nikicheza Biko kwa sababu ni mchezo mzuri maana hauna mlolongo mrefu, hivyo wakati nasubiria zawadi yangu kutoka Biko, nawashauri Watanzania wote kugombania gurudumu la Biko kwa sababu kila mtu anaweza kushinda donge nono,” Alisema.
Baada ya kutangazwa kunyakua Sh Milioni 10, mshindi huyo anatarajiwa kukabidhiwa fedha zake mapema wiki hii kwa utaratibu wa kufunguliwa akaunti katika benki ya NMB sambamba na kupewa elimu ya kifedha kama walivyopatiwa washindi wenzake wa jijini Dar es Salaam.