Vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba SC, leo wamemtangaza kiungo wao Mzamiru Yassin kuwa ndiye mshindi wa Tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Machi mwaka 2017, ikiwa ni mara yake ya pili kutwaa tuzo hiyo ndani ya klabu.
Kiungo huyo Tuzo yake ya kwanza alishinda mwezi Oktoba mwaka 2016 kwa kupigiwa kura na mashabiki kutokana na jitihada na kujituma kwa timu yake pindi wanapokuwa dimbani na hatimaye kuipa ushindi.
Kiungo huyo Tuzo yake ya kwanza alishinda mwezi Oktoba mwaka 2016 kwa kupigiwa kura na mashabiki kutokana na jitihada na kujituma kwa timu yake pindi wanapokuwa dimbani na hatimaye kuipa ushindi.
Ikumbukwe, mchakato wa kumpata mchezaji bora wa mwezi hupatikana kwa mashabiki wa Simba kuanza kupendekeza jina la mchezaji wanaomtaka kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii ya klabu hiyo na mwishowe huanza kupigiwa kura.
Kwa upande mwingine, leo timu ya Simba SC itashuka dimbani kuvaana na Wanalambalamba (Azam FC) katika kutafuta tiketi ya kuingia Fainali michuano ya Kombe la Shirikisho FA, utakaochezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.