Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage amekiri kupokea taarifa za katazo lililotolewa na serikali ya Kenya juu ya uuzwaji wa gesi zinazotumika majumbani zinazotoka Tanzania na kusema wataalamu wa wizara wanazifanyia kazi taarifa hizo.
Waziri Mwijage ametoa taarifa hiyo wakati alipozungumza na mwandishi wahabari wa Azam Two mjini Dodoma baada ya kuzagaa kwa taarifa za serikali ya kenya kupiga marufuku ya gesi zamajumbani za Tanzania kuuzwa Kenya na kukiri kuwa Kenya wamekuwa na chokochoko kadhaa lakini watahakikisha wanakaa chini kutafuta suluhu ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha viongozi wa juu wa nchi hizi mbili.