Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

UMOJA NI NGUVU NA UTENGANO NI UDHAIFU

$
0
0
Na Mwandishi wetu, Vijimambo Blog
Nimekuja tena leo nimaitumaini yangu kuwa wote hamjambo na kwa kudra zake mola mtakua mnaendelea vyema na mihangaiko ya kila siku.

Na kama nilivyoandika wiki mbili zilizopita kuhusiana na swala la uraia pacha na katika kuchunguza kwangu maisha ya DIASPORA hasa WaTanzania nimegundua umoja wetu katika kulipigania swala hili la uraia pacha ni mushkeli, nadhani ni kutokana na tofauti tulizo nazo katika mafanikio na nafasi ya kila mmoja wetu ughaibuni na wengine kutoona umuhimu wa swala zima la uraia pacha.

Kuna aina mbili ya Watanzania DIASPORA, kwanza ni wale Watanzania ambao wanaishi nje ya Tanzania na bado wanashikilia pasi za kusafiria za Tanzania na kundi la pili ni lile la WaTanzania waliobadili uraia wao kwa ajili ya kubanwa na sheria za ukaazi wa nchi walizopo, kundi hili la pili kisheria halitambuliki kama Tanzania DIASPORA kwani ni raia tayari wa nchi walizochukua uraia. Tofauti hizi ndio kikwazo kikubwa cha umoja na mshikamano wa msukumo na nia ya kupigania uraia pacha.

WaTanzania ambao bado wanapasi za kusafiria za Tanzania ukumbuke kwamba swala hili la uraia pacha ni kwa faida ya vizazi vyetu unapolipuuzia ulitendehi haki swala lenyewe wakiwemo watoto wetu ambao wanapozaliwa ughaibuni uwezekano ni mkubwa wa kuchukua uraia wa nchi aliyopo na nchi kama Marekani watoto wakibahatika kuzaliwa huko wanakua raia moja kwa moja.

Kitu kitakachosaidia kwa mtoto kurithi mali zako Tanzania ni swala hili la uraia pacha litakapopatiwa ufumbuzi. Japo kuwa wewe unaefikiria halikuhusu kwa sababu tu hujabadili uraia lakini una miaka zaidi ya 20 unaishi ughaibuni na una watoto hiyo ni kujidanganya, pigania uraia pacha upatikane ili mali zako zisipotee kwani sheria iliyopo sasa kama wewe sio raia wa Tanzania huwezi kumiliki ardhi, kesho na keshokutwa usipokuwepo nani atarithi mali zako Tanzania? kama sio mtoto wako ni nani tena. Tupiganie kwa pamoja swala hili ni letu sote.

Pamoja na kwamba baadhi ya WaTanzania  wamebadili uraia kumbuka kwa huo ni kwenye karatasi tu asili yao ya kuzaliwa daima itabaki Tanzania. Ni haki ya kila mmoja wetu kupigania kwa nguvu zote, wenzetu Kenya iliwachukua zaidi ya miaka 20 mpaka serikali yao kukubali uraia pacha ipo siku serikali yetu sikivu itaona umuhimu wa uraia pacha na kuwezesha kufanikisha swala hili lakini ukumbuke umoja wetu ndio utakaokua nguzo kuu ya mafanikio haya.

Nakupa mfano mdogo hapa juzi kati kulitokea WaTanzania kuja na wazo la kuanzisha umoja wa WaTanzania Duniani kwa lengo kuu la kupigania uraia pacha na haki za WaTanzania wanaishi nje ya nchi yao, wazo lao ni zuri kama yalivyokua mawazo mengine ya kuanzisha jumuiya zilizopita japo kila chenye mwanzo hakikosi changamoto zake na mimi mwenyewe nilifikiri changamoto zingetokea Tanzania lakini kinyume chake changamoto nyingi zimetokea kwa WaTanzania waishio ughaibuni wakikiwemo baadhi ya WaTanzania wenye Jumuiya zao nchi zilizopo kupiga vita za makusudi kwa lengo la kukwamisha jitihada hizi na kusahau kwamba umoja umeundwa ili kuunganisha nguvu ya WaTanzania Duniani.

Umoja huu haukua na lengo ya kuua jumuiya zingine za WaTanzania zilizoanzishwa hapo nyuma kwenye nchini zao kama inavyofikiriwa na baadhi ya wadau ughaibuni, Lengo kama nilipokutaarifu hapo mwanzo ni kuunganisha nguvu ya pamoja ikiwemo juhudi na mawazo za jumuiya hizo ilizoanzisha awali ya kupigania uraia pacha UMOJA NI NGUVU NA UTENGANO NI UDHAIFU kama nia yetu ni moja kwanini tunatofautiana na kulumbana kwa hili? Bila ya sisi kuondoa tofauti zetu na kuwa kitu kimoja Uraia pacha utachukua muda mrefu zaidi kwa serikali kutuelewa.

Mfano mwingine ni wakati tume ya Warioba ilipokua ikitafuta maoni ya katiba pendekezwa, Diaspora pamoja na kwamba tunakadiriwa tupo zaidi ya milioni 2 lakini waliotoa maoni hawakuzidi elfu sitini, hii ni jinsi gani sisi wenyewe hatuoni umuhimu wa hili swala inabidi tubadilike tuunganishe nguvu ya pamoja popote pale ulipo nje ya Tanzania aidha wewe ni raia wa nchi nyingine au bado unashikilia pasi ya Tanzania kumbuka atakae kula matunda ya jasho lako ni kizazi chako, acha watoto wakukumbuke kwa hili kwamba ulilisimamia kwa ajili yao.

Naomba kwa leo niishie hapa.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu ibariki Diaspora.





Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>