Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo amewaapisha Katibu na naibu katibu wa Bunge Maalum la katiba katika hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu ndogo mjini Dodoma leo.
|
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Katibu wa Bunge Maalum Mhe Yahya Khamis Hamad. Wa pili kushoto akishuhudia ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na watatu kushoto ni karani wa Baraza la Mawaziri Bwana Gerson Mdemu Dkt. Thomas Kashililah akila kiapo kuwa Naibu Katibu wa Bunge Maalum la Katiba.Wa pili kushoto akishuhudia kiapo ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na watatu kushoto ni karani wa Baraza la Mawaziri Bwana Gerson Mdemu.
|
|
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa serikali na viongozi wa bunge maalum la katiba muda mfupi baada ya kuwaapisha Katibu na Naibu Katibu wa Bunge hilo katika hafla iliyofanyika ikulu ndogo mjini Dodoma leo. Kutoka kushoto ni Katibu wa Bunge maalum la Katiba Bwana Yahya Khamis Hamad,Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue. Waziri Mkuu Mizengo Pinda ,Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mh.Samuel Sitta,Makamu Mwenyekiti wa Bunge maalum la Katiba Mh.Samia Suluhu, Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Sefu Iddi, Naibu Katibu wa Bunge Maalum Dkt.Thomas Kashilila na kulia ni Mwenyekiti wa muda wa Bunge maalum la katiba aliyemaliza muda wake Mh.Pandu Ameir Kificho. Picha na Freddy Maro. |