Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harison Mwakyembe akizungumza na uongozi wa Simba ukiongozwa na Rais wake Bw. Evans Aveva Mjini Dodoma.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Simba ukiongozwa na Rais wake Bw. Evans Aveva Mjini Dodoma. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WHUSM Dodoma.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe amekutana na na uongozi wa klabu ya Simba ukiongozwa na Rais wake Bw. Evans Aveva kwenye Ofisi zake Mjini Dodoma.
Uongozi wa Simba umeitikia wito wa Mhe. Mwakyembe wa kukutana naye na kujadili masuala mbalimbali ya mpira wa Miguu zikiwemo fursa na changamoto katika mabadiliko na maendeleo ya uendeshaji wa timu.
Aidha Mhe. Mwakyembe amepokea maoni ya Uongozi wa samba na kusahauri kuendelea kutoa ushirikiano na wadau wa mpira wa miguu nchini.
Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara husika prof Elisante Ole Gabriel, Mkurugenzi wa Michezo Yusufu Omary, Katibu Mkuu wa BMT Mohamed Kiganja, na Msajili wa Vilabu na Vyama nchini.