Mkurugenzi wa kituo cha mazoezi ya Bodyline Health &Fitness, Abbas Jaffer Ali (katikati) akiongea na waandishi wa habari wakati akitangaza tamasha la michezo linalotarajiwa kufanyika Aprili 22, 2017 Mayfair jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Katibu Mkuu - Shirikisho la Watunisha Misuli Tanzania, Francis Mapugilo (kulia) na mwalimu wa mazoezi.
Kituo cha mazoezi cha Bodyline Health& Fitness kimeandaa tamasha la mazoezi litakalofanyika kesho jumamosi Mayfair Msasani jijini Dar es Salaam.
Akizungumza mkurugenzi wa Bodyline Health& Fitness, Abbas Jaffer Ali alisema kuwa lengo la tamasha hilo ni kuwajenga watanzania wapende kufanya mazoezi ili kuimalisha afya zao.
Aliongeza kuwa katika tamasha hilo kutakuwa na michezo mbali mbali ikiwemo shindano la kutunisha mishuli, kuogelea na viungo vya mwili.
Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano.
Katibu Mkuu - Shirikisho la Watunisha Misuli Tanzania, Francis Mapugilo (katikati) akisisitiza watzania kujitokeza kwa wingi kushiriki mazoezi.
Baadhi ya washiriki wa mchezo wa kutunisha misuli wakionyesha umahili wao.