Msanii wa miondoko ya 'HipHop' nchini Tanzania, Kala Jeremiah awachana wasanii wenzake kuwa waache tabia ya kuharibu misingi ya 'HipHop' kwa kutunga nyimbo zenye mashairi ya kujisifia vitu walivyokuwa navyo na kusahau misingi ya muziki huo
Kala Jeremiah amebainisha hayo baada ya kelele za wadau wengi wa muziki wa aina hiyo kudai wasanii wengi wa kizazi hiki wanashindwa kuimba nyimbo zenye kuleta ujumbe wenye uhalisia katika jamii na matokeo yake wengi wanaangukia kwenye mashairi yasiyokuwa na tija.
"Kwangu mimi naamini 'Hip hop' ni kitu kinachotakiwa kije na ujumbe au kiwe na kitu fulani ndani yake, 'actually' ilikuwa hivyo zamani hapa bongo, yaani wimbo unakuta una ujumbe mzuri ambao unalenga jambo moja kwa kulichambua kwa kina, yaani hadi msikilizaji anapata hamu ya kushawishika kurudia na kurudia. 'Hip hop' ni uhalisia". Alisema Kala Jeremiah
Aidha msanii huyo aliendelea kuwachana kwa kusema marapa wengi wa bongo siku hizi hawaeleweki wanaimba nini ?, wanakazi ya kuwachanganyia vitu mashabiki
Kwa upande mwingine msanii huyo amewasisitizia wasanii wote kuzingatia nguzo za muziki wanaofanya na endapo wanataka kufanya biashara basi itakuja baada ya kufanya kazi nzuri.