Wakati ambapo China imepeleka angani satellite 10 kuitafuta ndege ya Malaysia Airlines iliyopotea, serikali ya Malaysia imewaomba waganga wa kienyeji kusaidia zoezi hilo.
Mganga maarufu nchini humo Ibrahim Mat Zin anayejulikana kama ‘Raja Bomoh Sedunia Nujum VIP’ alifanya tambiko kwenye uwanja wa ndege Kuala Lumpur Jumatatu hii kusaidia kuitafuta ndege hiyo ya MH370. Anadaiwa kuitwa na viongozi wa juu wa serikali.
“Nadhani ndege bado ipo angani ama ilianguka baharini,” alisema Ibrahim Mat Zin.