|
Mhe.Samia Suluhu Hassan (anaye angalia kamera)akipongezwa na aliyekuwa mshindani wake Mhe Amina Abdalla Amour mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi.
Hatimaye leo Bunge maalum la Katiba limemchagua Mhe.Samia Suluhu Hassan kuwa Makamu Mwenyekiti wake mjini Dodoma. Hii inakuja baada ya jana kumchagua Mhe.Samweli Sitta kuwa Mwenyekiti. Mhe Hassan alichaguliwa kwa kura 390 sawa na asilimia 74.6 na kumshinda mpinzani wake Amina Abdalla Amour. Kura 7 ziliharibika - kama jana. |
|
Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Maalum la Katiba mteule Dodoma, akishukuru wajumbe kwa kumchagua Katibu wa Bunge hilo Maalum ambaye atajulikana wakati wowote kuanzia sasa ataapishwa na Rais Jakaya Kikwete kesho asubuhi Ikulu ndogo Dodoma. Katibu wa Bunge ndiye atakayemwapisha Mwenyekiti na Makamu wake, na Mwenyekiti atawaapisha wajumbe wote, ndipo shughuli itapoanza rasmi ya kuandika katiba mpya. ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI |
Wajumbe kinamama wakishangilia mara baada ya Bunge Maalum la Katiba kumpata Makamu Mwenyekiti Mhe.Samia Suluhu Hassan mjini Dodoma leo
Hoi hoi na nderemo
Chereko chereko...
Picha na Deusdedit Moshi wa Globu ya Jamii, Dodoma