Wafanyabiashara ya Madini ya mchanga,kokoto na mawe Jiji la Mbeya wameandamana kwenda ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji kwa kutumia maroli kupinga waraka wa Wizara ya Nishati na Madini unaowataka watumiaji wa bidhaa hiyo kulipia shilingi elfu mbili mia tano kuanzia Machi 3 mwaka huu.
Maandamano hayo yalipokelewa na Mkurugenzi wa Jiji Mussa Zungiza ofisini kwake ambapo alikana kutoa waraka huo na kufafanua kuwa waraka huo umetolewa na Wakala wa Ukaguzi wa Madini[Tanzania Minerals Audit Agency-TMAA].
Akitoa malalamiko yao mbele ya Mkurugenzi Bwana nidhamu wa wachimbaji na wasafirishaji bidhaa hizo Peter Hezron N’gwavi amesema kuwa kitendo cha tozo na leseni kitafanya vijana waliojiajiri kuanza kufanya vitendo vya uhalifu kutokana na ukosefu wa mitaji.
Mkurugenzi wa Jiji amesema kuwa madai yao hayahusu ofisi yake bali wenye dhamana ya kujibu kero hizo ni mamlaka husika ambayo ni Wizara ya Nishati na Madini hivyo atawaomba wawakilishi wao waweze kujibia kero zao.
Mhandisi wa Jumanne Mohammed ambaye ni Afisa Mfawidhi ofisi ndogo ya TMAA Mbeya amesema kuwa waraka wa kulipia bidhaa za Mchanga,Kokoto na Mawe ulipitishwa na Bunge Mwaka 2010 ndipo ulipoanza kutumika rasmi kwa tozo la asilimia 3 kwa bei ya bidhaa iliyopo Sokoni.
Hata hivyo Mohammed amesema kuwa leseni za uchimbaji wa bidhaa za ujenzi hazihusiani na madereva wanaobeba bidhaa hiyo hivyo wao wanapobeba bidhaa hizo wanapaswa kupata kibali kuoka kwa mmiliki wa mgodi wa madini hayo ambapo kibali hicho hutolewa bure katika ofisi yake iliyopo eneo la Mwanjelwa Jengo la IFAD.
Alimaliza kwa kuwataka wanaotaka kufanya biashara hiyo wafuate taratibu za kisheria ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima kwani hali hiyo inaikosesha Serikali pato halali linalotokana na watu wachache wanaojinufaisha bili kufuata taratibu.
Na Mbeya yetu
|