NDEGE ya shirika la Ndege la Malaysia aina ya Boeing 777 iliyotoweka jana asubuhi bado haijapatikana mpaka sasa. Ndege hiyo iliyokuwa imebeba abiria 227 na wafanyakazi 12 kutoka nchi mbalimbali ilipoteza mawasiliano saa moja baada ya kupaa kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kuala Lumpur, Malaysia ikielekea Beijing, China.
Vikosi vya uokoaji kutoka nchini China vikielekea eneo inapodaiwa kuzama ndege ya Malaysia aina ya Boeing 777.
Baadhi ya ndugu wa abiria waliokuwa kwenye ndege iliyopotea wakilia kwa simanzi baada ya taarifa za kupotea ndege hiyo.
Meli ya ulinzi ya Vietnam ikiwa kisiwa cha Phu Quoc inapohofiwa kuzama ndege hiyo.
Meli ya ulinzi ya Vietnam ikiwa kisiwa cha Phu Quoc inapohofiwa kuzama ndege hiyo.
Taarifa zinadai ndege hiyo ilianguka katika bahari karibu na visiwa vya Phu Quoc, Vietnam. Zoezi la kutafuta ndege hiyo bado linaendelea katika visiwa hivyo.