Rais wa Serikali ya Wanafunzi CBE Dodoma, Bw. Remidius Mwema Emmanuel akiwa katika Eneo la makole Tayari kushiriki zoezi la usafi katika Kata ya Makole, Mkoani Dodoma.
Baadhi ya Wanafunzi wa CBE pamoja na Marais wa vyuo vya Dodoma wa kielekea katika eneo jingine tayari kuendelea na zoezi la usafi.
Baadhi ya Wanafunzi wa CBE pamoja na Marais wa vyuo vya Dodoma wa kielekea katika eneo jingine tayari kuendelea na zoezi la usafi.
Hali ilikuwa hivi wakati Wanafunzi wakiendelea na zoezi la kufanya usafi
Spika wa Bunge la Wanafunzi (CBE), Bw. Frank Mshana (Anayeruka) akiwa na Fyekeo Mkononi tayari kuendelea na shughuli ya Usafi.
Rais wa Chuo Kikuu cha St. John, Bw. Katumbi Edmund . J. Akishiriki katika zoezi hilo la Usafi , lililo andaliwa na Serikali ya Wanafunzi Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE - Dodoma)
Makamu wa Rais wa Chuo kikuu cha Dodoma, Bw. Mahamudu Rashidi Hussein (Mkono wa Kulia) akishiriki kikamilifu katika zoezi hilo la kufanya usafi.
Wanafunzi wa chuo cha Elimu ya Biashara(CBE) Kampasi ya Dodoma chini ya Rais wao Bw. Remidius Emmanuel wamefanya usafi katika kata ya Makole.
Akizungumza na dhumuni la tukio hilo, Rais wa Serikali ya Wanafunzi Bw. Remidius amesema wameamua kufanya Usafi kama sehemu ya kudumisha mahusiano na jamii zinazokizunguka chuo hicho. Ingawa amepongeza kwa ushirikiano alioupata kutoka kwa Marais wa vyuo vya Dodoma ambao wameweza kushiriki katika zoezi hilo. Akiwatambua kwa majina , Amesema Marais hao ni pamoja na ,Bw. Mahamudu Rashidi Hussein (Makamu wa Rais UDOM) , Bernard Janus ( College of Social Sciences) , Kagombora Joanes (College of Earth Sciences) na Bw. Katumbi Edmund J. Rais wa Chuo kikuu cha ST. John Tanzania.
Katika hatua nyingine Viongozi hao wamekemea vikali tabia ya baadhi ya watu kutumia vibaya majina ya Vyuo vyao kwa nia ya kujipatia umaarufu ikiwa ni pamoja na kujenga dhana potofu dhidi ya Maadili ya wanafunzi wa vyuo vyao. Akizungumza kwa uchungu mkubwa Rais wa CBE Bw. Remidius amesema Baadhi ya wamiliki wa Blogu wamekuwa na tabia ya kutumia picha chafu kutoka mataifa mbalimbali na kisha kuandika kuwa ni wanafunzi wa vyuo vikuu , " Lazima ifike hatua ifahamike kwamba Blogu zina heshima yake na wapo watu wanaendesha maisha yao kupitia Blogu zao, hivyo nawaomba watu wachache wanao tumia Blogu zao vibaya kuacha mara moja kwani kwa kufanya hivyo wanaondoa dhana ya uwepo wa Blogu hizo" Alisema Rais huyo.
Kwa upande wake Rais wa St. John Bw. Katumbi Ameitaka jamii pia kuyazungumzia mazuri yanayofanywa na vyuo hivyo na sio kuwa na mtizamo hasi na dhidi ya vyuo vikuu pamoja na taasisi za Elimu ya juu.