Wanandoa wanaoishi Sierra Nevada nchini Marekani wamefanya uvumbuzi ulioshangaza dunia.Uvumbuzi huo ulitokea mara baada ya kukuta kibati kilichokua na kutu kikiwa kinachungulia aridhini katika uneo la nyumba yao. Ndipo walipoamua kuchukua vifaa na kuchimba ili kuona ilikua ni kitu gani.
Baada ya kuchimbua walikuta ndoo mbili ambazo zilikuwa na sarafu zipatazo 1,427 za dhahabu. Sarafu hizo za dhahabu zina thamani zaidi ya mamilioni ya dola za Kimarekani. Sarafu hizi inasemekana zilitumika kwenye karne ya 19.
CHANZO: MSN