Wafanyakazi wanawake kutoka ofisi mbalimbali wakiwa wamejipanga kwaajili ya kuanza maandamano hapo jana yaliyoanzia katika shule ya msingini mabatini iliyopo Wilaya ya Temeke na kuishia katika uwanja wa Mwembe Yanga, wakati wa maadhimisho ya Sikukuu ya Wanawake Duniani yaliyofanyika tarehe 8 Machi 2014.
Kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani wakksindikizwa na Bendi ya Polisi wakati wa maadhimisho ya Sikukuu ya Wanawake Duniani iliyofanyika Jana katika Uwanja wa Mwembe Yanga, Wilayani Temeke Jijini Dar Es Salaam.
Bendi ya Kikosi cha Kujenga Taifa nao wakiwasindikiza waandamaji katika Kilele cha Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika jana tarehe 8 Machi 2014 katika Viwanja Vya Mwembe Yanga, Wilayani Temeke, Jijini Dar.
ENDELEA KUTZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Wadau wa Mfuko wa PPF nao wakiwa katika Maandamano
Mgeni Rasmi Bi Hawa Ghasia (wa pili kushoto) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Mh Mecky Sadick na wageni wengine wakiwa tayari kuyapokea maandamano yaliyofika katika Uwanja wa Mwembe yanga jana wakati wa maadhimisho ya SIkukuu ya Wanawake Dunia.
Wakazi wa Temeke wakiwa Juu kushuhudia yaliyokuwa yakiendelea katika Viwanja vya Mwembe Yanga wakati wa Maadhimisho ya Sikukuu ya Wanawake Duniani yaliyofanyika tarehe 8 Machi 2014 katika viwanja hivyo
Magereza nao hawakuwa nyuma
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari nao wakishangilia siku ya wanawake duniani
Burudani ikiendelea..
Ungo ukipitishwa...Changia Unachoweza..
Burudani kutoka Kwa Mkuu wa Mkoa Wa Dar Es Salaam, Mh Said Mecky Sadick akisakata Rumba
Wadau wa PPF wakiserebuka
Doroth Kaiyuzi , Kutoka Chama cha Wasioona Akisoma Risala mbele ya Wageni Rasmi katika Maadhimisho ya Sikukuu ya Wanawake yaliyofanyika katika Uwanja wa Mwembe Yanga, Jijini Dar Es Salaam, tarehe 8 Machi 2014
Wakazi wa Jiji la Dar wakitembelea Mabanda mbalimbali yaliyopo katika uwanja huo wa Mwembe Yanga wakati wa Maadhimisho ya Sikukuu ya Wanawake Duniani hapo tarehe 8 Machi 2014.Picha Na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog