Abiria wakitoka kwenye gari hiyo baada ya kupinduka
Abiria wakisaidiwa na wasamaria wema kutoka kwenye gari hiyo
ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Wananchi wakiendelea kuwasaidia abiria hao ili kuwahishwa hospitalini kwa matibabu
Hapa abiria wengine wakijiokoa wenyewe kutoka kwenye gari hilo.
FRANK KIBIKI, IRINGA
ZAIDI ya watu kumi, wamejeruhiwa vibaya na kukimbizwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Iringa, baada daladala waliyokuwa wakisafiria kutoka Frelimo kwenda Tumaini, mjini Iringa kuacha njia na kuanguka.
Ajali hiyo imetokea mchana huu majira ya saa saba mchana, baada ya gari hiyo kushindwa kupanda mlima, na badala yake kurudi nyuma kabla ya kutumbukia kwenye mto.
Mwitikio imewashuhudia wasamaria wema wakiokoa majeruhi waliokuwa wamepanda daladala hiyo yenye namba za usajili, T 106 ABP ambao wote wamekimbizwahospitali kwa ajili ya matibabu.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Iringa, Ramadhani Mungi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo kwamba taarifa zaidi itatolewa baada ya uchunguzi kukamilika