Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

TAARIFA MUHIMU: SEMINA YA WAJUMBE WA BUNGE MAALUM IMEAHIRISHWA MPAKA SAA TISA MCHANA LEO.

$
0
0

  Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Askofu Mstaafu Donald Mtetemela akiongoza sala ndani ya ukumbi wa Bunge leo Mjini Dodoma.


Kikao cha semina ya wajumbe wa Bunge maalum la Katiba kilichokuwa kiendelee leo saa nne asubuhi baada ya Mwenyekiti wake wa Muda Mhe. Pandu Amir Kificho Kuaarisha jana mchana sasa kitaendelea leo tarehe 8 machi 2014 saa tisa alasiri. 

Hii ni kutokana a kamati ya maridhiano inayopitia vifungu ilivyokuwa inafanyia kazi kuomba mda zaidi.Hivyo wajumbe wote wa Bunge maalum wanaombwa kufika Bungeni kuendelea na semina hiyo saa tisa alasiri badala ya saa nnne asubuhi.

Imetolewa na: 
Katibu wa Baraza la wawakiliashi 
na 
Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania



Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>