Ajali mbaya ya basi la kampuni ya AM Coach lenya namba T 763 AYN imetokea mkoani Tabora baada ya basi hilo kugongana na lori mali ya kampuni ya soda ya Coca Cola lenye namba za usajili T 256 BPP
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa na mmoja wa abiria aliyenusurika kwenye ajali hiyo ni kama ifuatavyo:-
"Dereva wa lori kajaribu kutukwepa lakini ufinyu wa barabara, mbele kuna lori scania linakuja,kwa hiyo akajikuta kagonga kushoto kwake na kulia kwake ila lori la kushoto kwetu halikusimama
Dereva wetu akashindwa kurudi upande wa kushoto kwa sababu kulikuwa na lori ambalo alikuwa anataka kulipita, basi letu lilikuwa 'linaovertake'(linataka kupita), basi nia AM Coach na lori ni la Coca Cola"