Leo blog hii ya Pamoja Blog ilifanikiwa kumnasa kijana mmoja wa mtaani ambaye alikuwa anaosha vioo vya magari kwenye foleni ya makutano ya barabara ya Morroco road, Alli Hassan Mwinyi, Mwai Kibaki na Barabara ya Bagamoyo akiwa hana hata shati na mvua ilikuwa ikinyesha. Hii ilionekana kama ni kuhatarisha maisha yake kwani magari yakiruhusiwa anaweza kugongwa na licha ya ilo afya yake inaweza kuwa mbaya zaidi.
Kijana huyo akielekea kwenye gari mojawapo lililokuwa liko kwenye foleni kwa ajiri ya kulisafisha kioo cha gari. Na pia barabara hii inatumiwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa inamaana hawaoni vijana hawa maana eneo hili kuna watoto wenye umri wa miaka minne na wanafanya kzi hizi za kuosha vioo vya magari.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Kijana huyu akisafisha kioo cha moja ya magari yaliyokuwa kwenye foleni hiyo.
Selikari isipoona tatizo hili watakao umia zaidi ni wananchi maana kwa hali kama hii tunatengeneza bomu kubwa ambalo litalipuka vibaya kwani ndani ya hawa watoto ndo wanazaliwa majambazi na hata vibaka
Akimalizia kusafisha kioo hicho cha gari na alipomaliza kusafisha alielekea upande wa dereva na kupewa shilingi mia tano za kitanzania.
Baada ya taa za kuongozea magari ziliporuhusu kwenye barabara ya Ali Hassan Mwinyi alianza kupishana na magari ili kufika katikati ya barabara inapotenganisha magari yanayopanda na yanayoshuka
Kijana huyo akielekea kwenye sehemu yake ili kuweza kuyapisha magari na baada ya magari kusimama tena aliweza kuendelea kufanya kazi hizo za kusafisha vioo vya magari.
PICHA NA PAMOJA BLOG