Meneja wa Mradi wa Kusaka Vipaji Vya Uigizaji Tanzania (Tanzania Movie Talents) Bw Joshua Moshi akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wakutambulisha kampeni mpya ya kusaka Vipaji vya uigizaji kutoka kampuni ya Proin Promotions Limited mapema leo katika Ofisi za Proin Promotions Limited, Mikocheni, Mtaa wa Ursino, Pembeni ni Meneja Masoko wa Proin Promotions Limited Bw Evance Stephen
Meneja Masoko wa Proin Promotions Limited, Bw Evance Stephen (katikati) akielezea jinsi ya Kampuni ya Proin Promotions itakapozunguka katika Mikoa ya Tanzania Kwaajili ya Kusaka Vipaji vya Uigizaji Tanzania kwenye Mkutano na waandishi wa Habari mapema leo katika Ofisi za Proin Promotions Limited, Mikocheni, Mtaa wa Ursino,, Shindano litaendeshwa na Kampuni ya Proin Promotions Limited.
Meneja Mradi wa Kusaka Vipaji vya Uigizaji Tanzania (Tanzania Movie Talents) Bw Joshua Moshi (wa kwanza Kushoto) pamoja na Meneja Masoko wa Proin Promotions Limited, Bw Evance Stephen wakisikiliza Maswali kutoka kwa waandishi wa habari wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo katika Ofisi za Proin zilizopo Mtaa wa Ursino Mikocheni
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Muigizaji wa Filamu za Kitanzania Single Mtambalike almaarufu Rich Rich ambae pia ni mmoja wa majaji katika Shindano la kusaka vipaji vya uigizaji lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents lililopo chini ya Kampuni ya Proin Promotions Limited akiongelea jinsi washindi watakavyopatikana katika shindano hilo linalotarajia kuanza tarehe 1 Aprili 2014
Mwandishi wa habari kutoka kituo cha Runinga Cha Channel Ten, Bw Fredy Mwanjala akiuliza swali kwa Meneja Mradi wa Tanzania Movie Talents, Bw Joshua Moshi (hayupo pichani) kuhusiana na Shindano la kusaka vipaji vya uigizaji nchini
Meneja Masoko wa Proin Promotions Limited, Bw Evance Stephen (wa kwanza kushoto) akionyesha stika za TRA ambazo zinaonyesha Uhalali wa filamu za Proin Promotions lakini Pia Wateja watakaonunua Filamu kutoka Proin Promotions wanatakiwa kutuma namba zilizopo kwenye stika hizo za TRA kwaajili ya kuweza kujishindia zawadi mbalimbali kutoka Proin Promotions kama Vile TV za Samsung na deki zake
Meneja Masoko Wa Proin, Evance Stephen akionyesha Muhuri wa Moto uliopo kwenye Kasha la Filamu kutoka Proin Promotions, Muhuri wa Moto, Kasha jembamba na Stika za TRA ndio vitu vitatu vinavyooshesha Uhalali wa Filamu kutoka Proin Promotions Limited
Wakijibu Maswali Kutoka Kwa Waandishi wa Habari