Na: Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linawashikilia watu nane (8) wanaojihusisha na uhalifu wa makosa mbalimbali ya uhalifu yakiwepo ya kumiliki silaha kinyume cha sheria, kupatikana na bangi pamoja na pombe ya moshi katika masako uliofanyika tarehe 04/03/2014.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP amesema katika Wilaya ya Kongwa amekamatwa mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la MALUGUSO S/O MUNZE, Mgogo, Mkulima wa MBANDE akimiliki silaha aina ya gobole bila kibali na ni kinyume na sheria ya kumiliki silaha hiyo.
Pia Kamanda MISIME amesema katika Wilaya hiyohiyo amekamatwa mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la NGELISHOM S/O LEGUMA mwenye miaka 40, Mkaguru, Mkazi wa Vihingo Wilayani Kongwa kwa kosa la kukutwa na kete kumi (10) za Bhangi pamoja na NGEMAUYU D/O JUMA mwenye miaka 34, Mgogo pamoja na NENELWA D/O OLOTI mwenye miaka 30 wote wakazi wa Ngomai Tarafa ya Mlali akiwa na Pombe haramu ya Gongo Wilayani Kongwa.
Aidha Kamanda MISIME ameongeza kuwa katika Wilaya ya Dodoma wamekamatwa LOTTI S/O SIPRIAN, SELEMANI S/O SAIDI, ABDALLAH S/O JUMA na JOHN S/O CHEREI wakiwa na misokoto 24 ya bhangi katika eneo la Chango’mbe.