Maiti ya mtoto huyo
Mtoto wa kiume anayekadiriwa kuwa na miezi 6 ambaye hajatambulika jina lake wala makazi amekutwa amefariki dunia kichakani baada ya kutupwa na mtu asiyefahamika katika kijiji cha Mhongolo wilayani Kahama
Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho Ally Manyama amesema kuwa baada ya kufika eneo la tukio alikuta mwili wa mtoto huyo ukiwa umeviringishwa katika kitenge na kutupwa kichakani katika eneo hilo.
Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limethibitisha kutokea kwa tukio hilo