Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

MAMBA ALIWA KILAINI NA CHATU NCHINI AUSTRALIA

$
0
0
 Nyoka huyo alijipinda kwa Mamba na kumbana hadi akafa
Chatu ameshinda vita vikali dhidi ya Mamba Kaskazini mwa mji wa QueensLand, kupigana na Mamba, kumpinda na kisha kumla.Tukio hilo lilishuhudiwa katika ziwa Moondarra, karibu na mlima Isa na kunaswa kwa kamera na wakazi wa eneo hilo siku ya Jumapili.Nyoka huyo mwenye urefu wa futi 10, alijipinda kwa Mamba na kuanza kupambana naye majini.Hatimaye, Nyoka huyo alifanikiwa kumshinda Mamba na kumtoa nje ya maji na kisha kumla.
Nyoka alimvuta Mamba na kumtoa ndani ya Maji
 Chatu ameshinda vita vikali dhidi ya Mamba Kaskazini mwa mji wa QueensLand, kupigana na Mamba, kumpinda na kisha kumla.Tukio hilo lilishuhudiwa katika ziwa Moondarra, karibu na mlima Isa na kunaswa kwa kamera na wakazi wa eneo hilo siku ya Jumapili.Nyoka huyo mwenye urefu wa futi 10, alijipinda kwa Mamba na kuanza kupambana naye majini.
Hatimaye, Nyoka huyo alifanikiwa kumshinda Mamba na kumtoa nje ya maji na kisha kumla.

 ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBFYA HAPA CHINI

 
 Chatu huyo alianza kumla Mamba na kushangaza wakazi
 Tiffany Corlis,mkazi wa eneo hilo, alishuhudia pambano hilo na kupiga picha hizi.
"lilikuwa jambo la ajabu sana, '' aliambia BBC"tulimuona Nyoka akipambana na Mamba , alifanikiwa kumpinda mamba na kumzunguza hasa katika sehemu ya miguu ya ili kumdhibiti.''"pambano lilianzia ndani ya maji. Mamba alikuwa anajaribu kuweka kichwa chake juu ya maji wakati mmoja ingawa Nyoka alikuwa amembana sana.''"baada ya Mamba kufa Nyoka alijikunjua, na kuja mbele ya Mamba huyo na kunza kumla,'' alisema Tifanny.
Baada ya mlo huo mkubwa Nyoka alijiendea zake
Bwana Corlis alisema kuwa ilimchukua Nyoka dakika kumi na tano kuma yule Mamba.
''Bila shaka Nyoka huyo alishiba vyema, na hatuui alikokwenda, baada ya mlo wake,'' alisema mama huyo ambaye hakutaka kusuburi kumuona Nyoka tena.Mtu mwingine aliyeshuhudia pambano hilo Alyce Rosenthal, alisema kuwa wanyama hao wawili walipambana kwa karibu masaa 5. Hatimaye wote walionekana kuchoka.''Sio kitu unachoweza kuona kila siku,'' alisema Alyce.

CHANZO: BBC SWAHILI

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>