Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

MAKANYAGIO YA NG'OMBE YALETA MTAFARUKO WILAYANI CHAMWINO MKOANI DODOMA

$
0
0
 Wafugaji wa jamii ya Kisukuma wa kijiji cha Mpwayungu, Wilayani Chamwino Mkoa wa Dodoma waliolalamikia kufanyiwa vitendo vya ubaguzi na kudaiwa malipo ya fedha kwa ajili ya makanyagio na uongozi wa kijiji hicho Kulia ni Sosoma Udoya akiwa na Samwel Nyuki
Samwel Nyuki akiwa nje ya ofisi ya Serikali ya Kijiji cha Mpwayungu alipokuwa amefungiwa na uongozi wa kijiji hicho siku 3 kwa madai ya kutakiwa kukubali kulipa 800,000 za makanyagio ya Ng'ombe wanaofugwakijijini hapo, mmoja wa viongozi hao alimfungulia baada ya kushtukia ujio wa mwandishi aliyefika kijijini hapo.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI


 Na John Banda, Chamwino
WAFUGAJI wa jamii ya kisukuma wameilalamikia serikali Wilayani Chamwino mkoani Dodoma kutokana na kitendo cha Afsa mtendaji naMwenyekiti wa kijiji cha Mpwayungu kufanya vitendo vya uonevu na wa
kuwatoza fedha kinyume na utaratibu huku wakiwabagua. Wakizungumza na Mwandishi wa Habari hizi aliyefika katika kijiji hicho ili kujionea hali halisi walisema vitendo hivyo vimekithiri kiasi cha kuwachosha kiasi cha wao kuamua kutafuta usaidizi toka maeneo mengine.
Mmoja wa wafugaji hao Sosoma Udoya alisema vitendo vya ubaguzi vimekuwa vikiongezeka kila uchwao huku vitendo vya uonevu kwa vijana wake kukamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi na viongozi wa kijiji hicho Afsa mtendaji Jairosi Milimo na Mwenyekiti wake Gabriel Hoya mpaka watakapolipa faini za Makanyagio.
Udoya alisema kuanzia waanze kukamatwa mpaka leo bado hawajawa na tafsri halisi ya neno Makanyagio ambayo wamekuwa wakilazimishwa kulipia fedha mara dufu bila kupewa stakabadhi.
Alisema yeye wakati anaingia katika kijiji hicho mwaka 2012 alitozwa kiingilio cha shs laki nane [800,000] ambapo Aprl 2013 alilipa liasi kama hicho na kutokana na kutojua kusoma stakabadhi yake iliandikwa
400,000/= Aliongeza kuwa viongozi hao wamekuwa wakiwaandaa wanunuzi wa ngo'mbe
pindi wanapoenda kuwavamia hali inayowasababishia hasara ya mifugo yao kwani walazimishwa kuuza kwa kiasi kidogo cha fedha huku wakitishiwa kufukuzwa.
''Mwenyekiti Hoya huwa anakuja na gari yake akiwa na bunduki  mkononi huku akiwa kawaandaa wanunuzi wa Ng'mbe [MAGARAGAJA] katika maeneo tunayochungia akifika anasema nimekuja kuwakamata ili mlipe fedha za makanyagio eti wanyama hao wanakanyaga kwenye poli lake na ukubisha anawambia atawafukuza  mrudi usukumani, ''hivyo mnatakiwa kulipa kiasi cha fedha ambapo anaweza kusema laki
tano au zaidi na ukiwa huna wale hao jamaa wanalazimisha kununua ng'ombe wa 600,000 kwa 150,000 kwa hiyo unalazimika kuuza na akishapewa kiasi alichotaka wanaondoka huku wakiwaswaga'', alisema
Udoya.
Aidha alisema hivi karibuni alilazimika kuomba msaada na wasamaria wema wakamuonyesha kwa watu wa haki za binadamu baada ya mmoja wa vijana wake Charles Nyuki kukamatwa nyumbani akiwatoa Ng'ombe kwenda machungani  mwanzoni mwa wiki na kuswekwa kwenye ofisi ya kijiji kwa siku 3 akilazimishwa kulipa 800,000 ya makanyagio.
Walipotafutwa ili kutoa ufafanuzi Afsa mtendaji huyo na Mwenyekiti wake hawakupatikana kwenye simu kutokana na sababu za kimtandao na
hata meseji waliyotumiwa hawakuijibu Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo Adrian Jungu alisema hana taarifa hiyo na kwamba hawana kodi ya makanyagio  hivyo
atafika kijijini hapo kujionea hali ilivyo ili achukue hatua stahiki. ''Vitendo hivyo ni wizi naenda mwenyewe ili nikaonane nao nijue kwanini ikithi bika tu lazima wahusika niwafikishe mahakamani kwasababu hawawezi kutuchafulia halmashauri, sababu sisi hatuna kodi ya makanyagio na kama wana sheria ndogo ya kijiji lazima wangeileta
Halmashauri '', alimaka Jungu Stakabadhi NO 28464 iliyotolewa tarehe 21.04.2013  iliyodaiwa alikatiwa mmoja wa wafugaji hao Samwe Nyuki aliyedai kulipa 800,000 na kuandikiwa 400,000 kutokana na kutojua kusoma akilipia makanyagio ina kichwa Mapato ya serikali za vikijiji.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>