Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

AJALI YATOKEA MWEKA, MOSHI YAHUSISHA DALADALA NA LAND CRUISER

$
0
0
Ajali imehusisha gari ya abiria aina ya hiace inayofanya safari zake kati ya Mweka na moshi mjini  na landcruiser VX iliyokuwa  imewabeba  wanafunzi wa chuo cha usimamizi na uhifadhi wa wanyama pori Mweka kilichopo Mweka , Moshi vijijini.Kwa mujibu wa shuhuda wa ajali hiyo bwana Fred Mushi amesema kuwa gari aina ya landcruiser VX iligonga daladala  hiyo iliyo kuwa imesimama kupakia abiria kwenye kituo kimoja maarufu kwa jina la Kona. Ajali hiyo imetokea muda wa saa 10.30 jioni hii
 Daladala iliyogongwa vibaya na landcuriser ikiwa imeharibika vibaya ubavuni kiasi cha kutoweza kutembea tena lakini Taarifa za awali hali ya dereva wake   inasemekana kuwa mbaya pia idadi ya majeruhi mpaka tunaenda mitamboni  haijajulikana.tutaendelea kukujuza jinsi taarifa zitakavyofikia kuhusu hali na idadi Ya majeruhi. 
ENDELEA KUSOMA HABARI JII KWA KUBOFYA HAPA CHINI


Gari aina ya landcruiser VX iliyokuwa na wanafunzi toka chuo cha Mweka
ikiwa imezama kwenye mtaro  na kuharibika vibaya baada ya ajali hiyo mbaya iliyotokea jioni hii
mashuhuda walikokuwa eneo la tukio wakilitazama gari aina ya landcuriser iliyokuwa imezama kwenye mtaro baada ya ajali hiyo iliyotokea jioni hii na kusababisha majeruhi

PICHA NA HABARI NA mdau WITO MSAFIRI

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>