Mwili wa mtoto John Mwapwani (4) aliyefariki majira ya asubuhi baada ya kutumbukia kwenye tundu la choo nyumbani kwao mtaa wa Sikanda kata ya Chemchem eneo la Ally Hassan Mwinyi ndani ya Manispaa ya Tabora ukiwa unapandishwa kwenye gari la polisi.
Inasemekana kuwa mtoto huyo mara baada ya kuamka asubuhi ,baba yake mzazi alimwambia aende chooni kujisaidia kama ilivyo ada kwa wazazi wafanyavyo kwa watoto wao,Mtoto John(4)alikwenda chooni.
Baada ya kimya cha muda mrefu kutawala baba wa mtoto huyo alielekea sehemu ya choo,lakini katika hali ya kusikitisha alikuta mwili wa mtoto huyo ukielea kwenye maji machafu akiwa tayari amepoteza maisha.