Hii ni sehemu moja tu ya Mlimani City Mall ambayo kuna mlinzi mmoja tu eneo la kupaki magari hii ni hatari sana kwa wananchi wanaokuja na magari yao eneo hili maana hakuna ulinzi wa kutosha. Hivi kweli mtu huyu mmoja anaweza kulinda eneo lote la Mlimani City au kuna mchezo unachezwa.
Sehemu hii pia haina mlinzi anayelinda magari yanayopaki Mlimani City Mall hii ni hatari kwa watu wenye magari yao maana wezi ni wengi eneo hili kutokana na kutokuwepo kwa ulinzi mzuri. Unaweza kujiuliza hivi kweli hakuna walinzi wa kutosha wa kukaa kwenye sehemu hii maana kwa siku magari yanayoingia na kutoka Mlimani City ni zaidi ya 400.
ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Hivi kweli uongozi wa Mlimani City Mall unafanya hata ukaguzi eneo hili kuona kama kuna tatizo, mpaka blog yetu hii ilipopita hapo na kuliona hili tatizo kwa wakati mdogo. Ukitizama katika picha hiyo ya hapo juu unaona hakuna walinzi sehemu hizo mbili . Hivi kweli wizi ukitokea eneo hili nani atarahumiwa kati ya uongozi na walinzi wa Mlimani City.
Huu ndio mwenekano halisi wa magari yakiwa yamepaki na kuna mlinzi mmoja kwa juu ambaye hawezi kuona magari yote kwa kupitia juu.