Mawasiliano huchukua zaidi ya asilimia sabini (70%) katika maeneo ya kazi, hivyo unahitaji kuongeza uelewa wako na namna unavyowasiliana na kuchukua taarifa kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine. Watu wengi wamekuwa wakikosana na wafanyakazi wenzao kila mara kwa sabu ya namna tuambavyo hawajui umuhimu wa kuwasiliana au hawakufundishwa hivyo hawajui mambo ya msingi katika kuwasiliana.
Hahuhitaji shahada ya udhamili kujua namna ya kuwasiliana na wafanyakazi wenzako, unahitaji uelewa mpana katika kuwasiliana. ili kuongeza upana wa mawazo na maamuzi katika kuwasiliana, jaribu kufuatilia vipengele vifuatavyo;
Mara nyingi tunapenda kusikika kuliko kusikiliza, hivyo kupoteza agenda ya mazungumzo mengi kwa sababu tulikuwa hatusikilizi wengine. Tumekuwa tukiangalia agenda zetu kuliko kuangalia mwenzako anajaribu kuongea nini na umsikilize kwa umakini.
ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
2. Usipambane na mleta habari au mjumbe wa hiyo habari
Tunahitaji kuelewa, uwezo wetu mwingi una mtizamo fulani wa kuchukulia mambo na kumtazama anayeongea au aliyeleta ujumbe na kutengeneza hukumu kwa anayeongea bila kuangalia ujumbe anaokupa kwa undani zaidi. Hivyo angalia ujumbe zaidi kuliko kuangalia kwanini ametumwa mjumbe huyu.
3. Epuka kusoma fikra za watu
Huwa tunahitaji watu watuchukulie kwa namna fulani, wakati huo hatutaki hao watu wajue sisi tunahitaji nini na namna gani tutaweza kupata hicho kitu. Kabla ya kufikiri kwamba watu wanajua jambo fulani, kitu cha kwanza anza wewe kutoa hoja yako ili upate mrejesho wa mada hiyo.
4. Acha Kulazimisha
Tungependa kukubaliana na watu wengine, mara nyingi tunapambana kuonyesha kwa kiasi gani sisi tuko sahihi. Jaribu kutafuta eneo ambalo mnaweza kukubaliana ninyi wote ili kupata matokeo makubwa zaidi.
Msemo wa kitaaluma
Steven Covey, mwandishi wa kitabu cha tabia saba za watu wenye utekelezaji mkubwa anaemia ” Tafuta kwanza kuelewa, ili uweze kueleweka” katika mawasiliano yoyote hakikisha unaelewa kwanza kabla hujaanza kujaribu watu wakuelewe.
Je kuna namna ambavyo unataka kuongeza uelewa wako wa kuwasiliana? Je unahitaji kufanya nini kuweza kupata matokeo mazuri katika mawasiliano yako na watu? Je utajuaje kana kwamba umefanikiwa unapowasiliana na watu?
Hayo ni moja ya maswali ambayo unahitaji kuyafanyia kazi, ili kuongeza ufanisi katika mawasaliano yako na watu wengine kazini, kwenye biashara na hata maisha binafsi.