Wakati watu wengi wanasema kazi ni nzuri, ni rahisi kujisahau na kubaki hapo hapo. Ingawa una watu wote na msaada unaohitaji , inawezekana umejenga marafiki na kazi umeshaizoea lakini wengine wetu kama sisi haturidhiki. Tunahitaji kazi inayotosheleza shauku yetu, kazi ambayo ni zaidi ya mshahara wetu .
Tunahitaji kazi ambayo ni sehemu ya maisha yetu, isiwe inayotulazimisha kwaajili ya kuishi tu, kufanya tu kazi kutoka Jumatatu mpaka ijumaa na kutumia wikiendi kupunguza uchovu na sumu za kazini. Kihisia na kiakili.
Fuatilia dondoo hizi chache kama kazi yako imegeuka kuwa mbaya:
Kitu kitakachokuwezesha kupata upenyo ni kukubali tu kwamba mambo hayaendi. Haijalishi mtu mwingine anahisi vipi, au anapenda nini, maisha ni wewe mwenyewe unayeweza kupata uzoefu. Kama unasikiliza watu wengine (hao watu ni kama watu wasipenda kujaribu na kufuata maisha yao wenyewe) unakuwa unajiuza kwa bei rahisi. Ni wakati wa kuacha kuishi maisha ya wengine na uanze kuishi maisha yako.
ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
2. Usiiache kazi ikutambulishe
Kukubali kazi nzuri ndo kitu unachofanya, lakini si vile ulivyo. Unatakiwa kujitofautisha kati yako na kazi unayofanya. Usifanye kazi muda wote na kusahau kuishi maisha mengine tofauti na kazi, muda wa kazi ni kazi na maisha yako ni ya kwako usichanganye.
3. Tambua kuwa Fedha ≠ Furaha
Kitu unachopaswa kujua kupata fedha nyingi sio sawasawa na kuwa na maisha mazuri. Mara nyingi kazi zinazolipa vizuri hufanya watu wasiishi maisha ya furaha na mazuri na kujikuta unasahau ndoto zako na maisha yako halisi kwa sababu unafanya kazi sana. Muda mwingi tunautumia kazini, mikutano ya kikazi,safari za hapa na pale hivyo tunasahau kuna maisha tunatakiwa kuishi. Fedha zinatusaidia sisi kupata vitu vizuri na kujitunza sisi na familia zetu lakini fedha peke yake haiwezi kutupa maisha ambayo tunaona tutakuwa tumeyaishi.
Kuondokana na kazi mbaya tunahitaji kujitengenezea mafanikio kwa mipango yetu wenyewe badala ya kukaa na kubweteka kazini. Fanya kazi inayoendana na malengo yako na itakayokusaidia kupata kile unachokihitaji bila kupoteza mwelekeo wako kimaisha. Hata kama kuna kazi unayoipenda hailipi kulingana na kazi nyingine, jiondoe katika mtego huo. Jaribu kutafuta furaha yako inapatikana wapi, maisha yako ni nini? Na malengo yako ni yapi? Je unaishi maisha ya wengine?