Moja ya nyumba zilizobomolewa jirani na soko la Kilombero ambazo ni mali ya halmashauri ya jiji la Arusha kupisha uwekezaji mkubwa.
Tinga likiwa kazini
Hatimaye Halmashauri ya Jiji la Arusha imeanza kubomoa nyumba zaidi ya 300 baada ya malumbano ya kisheria mahakamani, yaliyochukua muda mrefu.
Ubomoaji ulianza asubuhi chini ya usimamizi wa Mkuu wa Wilaya ya Arusha, John Mongela, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji, Elphas Mollel, wakuu wa idara mbalimbali za halmashauri ya jiji, huku polisi wakiimarisha ulinzi.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Ubomoaji ukiendelea
Tofauti na ilivyodhaniwa kungetokea upinzani mkali kutoka kwa wapangaji, hali ilikuwa ya utulivu, huku wapangaji wakikusanya vitu vyao ili visiharibiwe na tingatinga zilizokuwa zikibomoa nyumba hizo.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha, John Mongela alisema nyumba hizo zimejengwa miaka mingi iliyopita na kupuuza kauli za wapangaji kuwa wana haki ya kumilikishwa nyumba hizo kwa kuwa wameishi kwa muda mrefu.
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha,Elphas Mollel alisema Kata ya Levolosi eneo la Samunge jumla ya nyumba 56, Kata ya Kaloleni nyumba 198 na Kata ya Themi ni 84 zinabomolewa, ili kupisha uwekezaji mkubwa na wa kisasa..
Hata hivyo, alisema nyumba mbili hazitabomolewa kutokana na moja kuwa na utata wa kisheria ambayo mmiliki anadai kuuziwa na Wakala wa Barabara nchini (Tanroads), wakati nyingine alisema Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi aliitoa kwa mama mkongwe.