Lamborghini haipo kwenye biashara ya magari ya kifahari tu. Na sasa imetangaza smartphone zake ziitwazo Antares.
Simu hizi chache zimetengenezwa kwa kufuatisha umbo la gari hizo za kifahari na zinatumia mfumo wa Android 4.3 na zinakuja na 1.5 GHz quad-core processor, RAM yenye ukubwa GB 1, kumbukumbu ya ndani yenye ukubwa wa GB 32 na micro SD yenye ukubwa wa GB 32. Simu hizi zinauzwa $4,000 ambazo ni sawa na shilingi milioni 6.2.