Kama Bosi wako ana swali humuuliza nani kwanza? ni wewe? Kama kazi yoyote haijafanyika nani huulizwa? ni wewe? kama anataka kufanya maamuzi makubwa na ya msingi hapo ofisini, huchukua ushauri kwa nani? kama ni kwako, inamaanisha bosi anakutegemea sana hivyo uamuzi wako wa kuacha kazi hatoufurahia kabisa. Ingawa hakuna utakachokiongea hapo ili bosi hafurahi unapofanya maamuzi ya kuacha kazi, hapa ni baadhi mambo unayotakiwa kufanya kama unaamua kuacha kazi.
Tangaza kuondoka kwako Mapema
Inapofika wakati wa kuacha kazi au kuondoka wafanyakazi wengi huacha bila taarifa au kuogopa kutangaza, ikiwa hasa kwa mabosi wao wa karibu sana. Ukiwa katika hali ya kuacha kazi andika barua na useme waziwazi. Kwa wewe kusema mapema katika hali nzuri, kuwasilisha vyema na kuonyesha heshima kwa walio juu yako. hali hiyo inaonyesha unamheshimu bosi wako na kuongea naye uso kwa uso, kumtumia barua pepe na kuchapa nakala kumwekea mezani kwake.
ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Elezea ni kwanini unaondoka
Hakuna kitu Bosi wako atakwambia kitakachosababisha uendelee kubaki kama ulipanga kuondoka, mweleze ni kwanini umeamua kuondoka ambacho kitamsaidia mbeleni watu wasiache kazi mfululizo. Kama umepata fulsa nzuri zaidi na kama hakuna tatizo kwenye kazi yako ya sasa , na kama kuna changamoto umeona huwezi kuendelea nazo ongea kwa utulivu bila hamaki.
Kazi zako za sasa zipangilie vizuri
Je Bosi wako anajua una kazi ngapi mezani kwako? inawezekana anajua. Je anajua kila kitu kuhusu kazi hiyo? inawezekana hapana. Tengeneza fomu ya orodha ya kazi zote zilizoko mezani kwako na wapi zimefikia. Malizia viporo vyako bila ya kuulizwa kuonyesha kwamba unathamini ulichokuwa unakifanya vilevile kutokuharibu namna wanavyoweza kukuongelea wakati watakapoulizwa na mwajiri mpya anayekuchukua.
Mfundishe na kumwelekeza yule anayechukua nafasi yako
Bosi wako atajisikia vizuri unapoondoka kama umemfundisha vizuri yule anayechukua nafasi yako. Jitolee kumfundisha mtu mpya katika nafasi hiyo. Na kama unaweza kufanya hivyo mara baada ya kupokelewa kwa barua yako ya kuacha kazi itakuwa vizuri zaidi. Kama huwezi na una muda wa kukaa zaidi kidogo kumalizia kazi fikiria kwamba huu ni uamuzi wa busara sana.
Ondoka kwa amani na kuacha mambo yamekaa vizuri. Hapo utakuwa tayari kuacha kazi.