Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

UJENZI WA BARABARA WALETA ADHA KWA WASAFIRI WILAYA YA BAHI

$
0
0
Gari likionekana likijaribu kupita bila mafanikio  katika barabara inayonganisha vijiji sita vya wilaya ya Bahi, adha hiyo ya usafiri imetokana na kujengwa kwa kutumia udongo mifinyanzi katika kijiji chaTobai. (Picha na John Banda)
 Barabra hiyo inavyoonekana katika kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kinyesha hali inayosababisha wananchi wanaoishi katika vijiji zaidi ya sita kukwama kusafiri pamoja ma mzao ya biashara.

 ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
 
 Shimo lililochimbwa na kukata barabra ya Lukali kongogo  kwa ajili ya kutengeneza karavati bila kuwa na njia mbadala hali  iliyosababisha adha kubwa kwa usafiri  huku mkandarasi wa ujenzi wahuo akijiojitetea  kutosubili ili kukwepa hasara kwa kampni yake.
 Gari la mizigo likiwa limekwama katika barabara hiyo inayojengewa karavati kwa kufungwa bila kuweka njia mbadala kwa ajili ya safiri kutokana njia kuwa moja na kutumika na wananchi wa vijiji zaidi ya sita huku mhandisi wa Wilaya ya Bahi Josephu Mkinga akiifunga kwa masaa 48 ili kupisha ujenzi huo.

Na John Banda, Dodoma
Mkandarasi anayetengeneza barabara yenye urefu wa km 8 ashindwa kufanya kazi yake kwa ufanisi kiasi cha kusababisha barabara hiyo kufungwa kwa zaidi ya siku tatu huku ikisababisha usumbufu mkubwa kwa
wananchi Wilayani Bahi Mkoani Dodoma. Barabara hiyo inayounganisha kati ya vijiji vya Kongogo na Lukali inajengwa katika kitongoji cha Tobago ambapo matengenezo yake yalianza
tokea mwezi wa 10 mwaka uliopita ambapo hata hivyo imemlazimu mkandalasi aliyepewa tenda na Halmashauri hiyo kampuni ya NISPA CONSTRACTIN.
Akiongea katika eneo hilo Juma Mwaja alisema kumekuwa na usumbufu mkubwa katika eneo hilo kutokana na kutopitika tena baada ya mkandarasi kuamua kuikata barabra hiyo kwa kuchimba shimo kwa ajili ya
karavati bila ya kuweka njia mbadala ambayo magari ya kusafirishia abiria na mizigo yatapita.
Mwaja alisema tatizo hilo ambalo limewasababishia kero lina zaidi ya siku tano na kumekuwa na mzozo kati ya wafanyakazi wa kampuni hiyo na wenye magari mara baada ya magari kukwama katika eneo hilo kutokana na utelezi mkubwa unaosababishwa na udongo wa mfinyanzi uliotumika .kuijengea.
"Mimi ni mwenyeji wa kijiji hiki ninapajua sana katika eneo hili hasa mvua ikinyesha panakuwaje hivyo tulikuwa tumepanga mawe na magali yalikuwa yanapita na tulijaribu kuwashauri kabla ya kuanza matengenezo wao hawakutusikiliza wakaondoa yale mawe sasa mvua imenyesha wameikata kabisa sasa tunateseka'' alisema
Aliongeza kuwa kinachomshangaza ni kitendo hicho cha mkandarasi kutoweka njia mbadala wakati hiyo ndiyo barabara pekee inayotumika kuunganisha vijiji sita na makao makuu ya wilaya ya Bahi ambavyo
wananchi wake ni wakulima wa mazao ya biashara yakiwemo mpunga, ufuta, mahindi, alizeti na karanga.
Mhandasi wa Halimashauri ya Wilaya ya Bahi Josephu mkinga alisema ofisi yake imelipata tatizo hilo na anajua ukubwa wake na tayali imeshamtuma mtaaramu ili kusimaia na kutoa ushauri ili ujenzi wa
karavati hilo ukamilike haraka ili barabara ipitike ndani ya saa 48 na kwamba tatizo hilo limesababishwa na mvua ya saa 5 iliyonyesha mwanzoni mwa wiki.
Kwa upande wake mkurugenzi wa kampuni ya NISPA iliyopewa kandarasi ya utengenezaji wa barabara hiyo alisema taarifa hiyo ni ya kisiasa kwa sababu anmjua mlalamikaji ni mtu furani mwenye kibasi kibovuboviu kinachopita barabara hiyo, lakini ameamua kuikata shimo hilo bila njia mbadala kwa sababu yeye hakupewa na halimashauri fungu.
''Mimi ni mtendaji si mtu wa siasa Siwezi kusubili lolote kwa sababu kwa kufanya hivyo nakuwa nje ya mkataba hali itakayonisababishia hasara, kwa hiyo tumeikata hiyo barabara kisheria na ndani ya saa hizo
48 tuna uhakikika tutakuwa tayali kama hali ya hewa haitabadirika'',
alisema Vijiji ambavyo vimekubwa na adha hiyo ya kushindwa kusafiri ni pamoja
na Bankolo, lamaiti, lukali, tobai, kongogo na bahi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>