Elizabeth Michael 'Lulu' (katikati) akiwa na mama yake mzazi, Lucresia Karugila (wa pili kushoto) na Dk. Cheni (kulia) ndani ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo.
Leo February 17 kutoka Mahakama kuu kanda ya Dar es salaam, msanii wa maigizo nchini Tanzania Elizabeth Michael maarufu kama Lulu alikuwa akisomewa shitaka lake la kuua bila kukusudia msanii mwenzake wa maigizo Marehemu Steven Kanumba April 07 2012 eneo la Vatican.
Akisoma maelezo ya awali wakili wa serikali Monica Mbogo mbele ya Jaji anayesikiliza kesi hiyo Rose Teemba amesema mshtakiwa siku ya tukio kulikuwa na ugomvi kati ya marehemu na mshtakiwa na baadaye mshtakiwa aliondoka usiku wa saa sita baada ya marehemu kuanguka chumbani ambapo alfajiri ya April 07 majira ya saa 11 alfajiri Lulu alikamatwa eneo la Bamaga.
Kwa upande wake wakili Peter Kibatala ambaye anamtetea Lulu amesema wameridhishwa na sehemu kubwa ya maelezo ya awali ya mteja wao, ambapo kesi hiyo imeahirishwa mpaka itakapopangwa tena huku kila upande ukitarajia kuleta mashahidi watatu. Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie waliohudhuria leo mahakamani ni Dr.Cheni na Kajala.