*Aamua kuwatetea mawaziri mizigo
*Amshangaa Mbowe kulazimisha Serikali tatu
RAIS Jakaya Kikwete amewakingia kifua mawaziri mizigo huku akishangazwa na malumbano yanayoendelea kutaka wafukuzwe kazi.
Amesema kwamba, uamuzi wa kuitwa na kuhojiwa kwa mawaziri hao katika kikao cha Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CC), kulitokana na hoja zilizoibuka kwa wananchi na kwamba kuitwa kwao hakukumaanisha kwamba wanatakiwa kufukuzwa kazi.
Kutokana na hali hiyo, amesema mawaziri hao mizigo, wamepewa maelekezo ya utendaji kazi huku wakifuatiliwa juu ya utekelezaji wa maagizo ya chama.
Rais Kikwete alitoa kauli hiyo jana jijini Mbeya, alipokuwa akihutubia katika kilele cha miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM.
Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, alisema Kamati Kuu ya CCM imetimiza wajibu wake, hivyo Serikali inafanyia kazi mapendekezo yote yaliyotolewa.

“Pale mawaziri wanne walipoitwa na Kamati Kuu baada ya ziara ya Mkoa wa Ruvuma na Mbeya, matatizo yaliyohusu sekta zao yalizungumzwa na uamuzi kufanywa kuhusu hatua za kuchukuliwa.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
“Najua wapo watu waliotaka mawaziri hao wafukuzwe kazi, kwa vile halikufanyika hilo, basi likageuzwa kuwa suala la malumbano, ni vema ieleweke kuwa, kuitwa kwao katika Kamati Kuu hakuna maana ya wao kufukuzwa.
“Wao waliitwa kwa sababu ya kuwepo matatizo yaliyoonekana yanatakiwa yapatiwe ufumbuzi, yamezungumzwa na maelekezo yametolewa kuhusu cha kufanya.
“Kamati Kuu imetimiza majukumu yake na uliobaki ni wajibu wa Serikali, Kamati Kuu itaendelea kufuatilia na kama hakuna maendeleo, inaweza kuchukua hatua zipasazo dhidi ya mhusika na huko hatujafika,” alisema Rais Kikwete.
Kauli ya Rais Kikwete inakuja katika kipindi ambacho kumekuwa na mijadala kuhusu uteuzi wa baraza lake la mawaziri, hasa baada ya mawaziri walioonekana kupwaya katika utendaji kurejeshwa tena katika baraza lake.
Akerwa na malumbano
Rais Kikwete, alikemea malumbano yanayoendelea ndani ya CCM huku akiwataka wanachama na viongozi kulipa uzito unaostahili suala la uadilifu wa viongozi na wanachama.
Kwa kufanya hivyo, alisema CCM inaweza kuwa imara na Serikali yake ikatekeleza majukumu yake ipasavyo na kwamba kama isipoungwa mkono inaweza kupoteza ushindi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa na uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
“Nataka tufanye kila linalowezekana tuondokane na tabia ya kutoa na kupokea rushwa katika kuchagua viongozi na mchakato wa uteuzi wa wagombea.
“Kamwe tusikubali uovu huu ukageuka kuwa mila na desturi ndani ya chama kikubwa chenye historia iliyotukuka kama CCM.
“Vitendo hivi lazima tuvikatae na tuvipige vita kwa nguvu zetu zote, tusiwaache watu wachache wanaotaka uongozi kwa gharama yoyote waharibu sifa nzuri ya chama chetu,” alisema na kuongeza:
“Tusiache ikajengeka dhana potofu, kwamba ukitaka uongozi ndani ya CCM uwe na fedha za kuhonga watu, tusikubali chama chetu kifikishwe huko,” alisema.
Kwa mujibu wa Rais Kikwete, watu hao wakiachwa waendelee na tabia hiyo, watakitoa thamani chama hicho mbele ya watu.
Alisema umefika wakati wa kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa katiba na kanuni za maadili ya CCM.
“Wale wote wanaofanya vitendo hivyo na mawakala wao, wathibitiwe na Kamati ya Maadili kwani ajizi ni nyumba ya njaa, tuchukue hatua haraka,” alisema.
Hata hivyo, Rais Kikwete alimpongeza Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwa kazi anayofanya ya kuimarisha chama, huku akiwataka viongozi wa ngazi zote kuiga mfano huo.
Alisema Kinana amekuwa akifanya mambo ambayo hayajawahi kufanywa na hata kutoa njia namna ya kufanya kazi ya chama ndani ya umma.
Alisema Kinana amekuwa akitoa fursa kwa wananchi kueleza matatizo yanayowasibu, ambapo hali hiyo imesaidia kumaliza matatizo akiwa mikoani.
“Pale ambapo panahitaji hatua zaidi za Serikali, hakusita kuwasiliana na Waziri Mkuu, vile vile amekuwa akitoa taarifa ya ziara zake kwenye Kamati Kuu ya CCM,” alisema

Amvaa Mbowe
Katika mkutano huo, Rais Kikwete alimvaa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na kusema kuwa amesikitishwa na kauli aliyoitoa kwamba, wao watatumia ngumi ili Katiba Mpya ipatikane.
Alisema kwamba, huenda Mbowe amekosa ukomavu wa kisiasa, kwani suala la uamuzi wa muundo wa Serikali tatu au Serikali mbili, litaamuliwa kwa hoja na siyo kwa kutumia mabavu.
Rais Kikwete, alisema uamuzi wa aina ya muungano unaofaa, utafanywa kwa hoja ndani ya Bunge la Katiba na kisha kupigiwa kura na wananchi, hivyo haiwezekani suala hilo likafanywa kwa mabavu.
“Ni matumaini yangu kuwa, kila upande utatumia hoja zenye nguvu kushawishi na kufanikiwa kuungwa mkono na upande wa pili. Nimesikitishwa na kauli ya Mbowe, kuwa watatumia hata ngumi ili wakubaliwe mfumo wa Serikali tatu, sijui ni kukosa ukomavu wa kisiasa au ni kitu gani.
“Jambo la wengi utalilazimishaje kwa ngumi? Jawabu ni kujenga hoja zenye mashiko na kwa umahiri mkubwa, ili wenzako wakuelewe na kukukubali, kutumia nguvu hakutasaidia na wala sio njia bora ya kutunga Katiba,” alisema.
Aliwataka wajumbe wa Bunge la Katiba, kufanya kazi yao kwa umakini na uadilifu, ili kuipatia nchi Katiba nzuri inayotekelezeka, itakayoimarisha muungano badala ya kuudhofisha.

Mgogoro Ziwa Nyasa
Rais Kikwete, alisema hivi sasa wananchi walioko kando ya Ziwa Nyasa hawastahili kutishwa, kwani ufumbuzi wa jambo hilo unasubiri Kamati ya Rais mstaafu wa Msumbuji, Joachim Chisano pamoja na Festus Mogae wa Botswana, ambao ndio watakaoeleza ukweli wa jambo hilo.
“Kwa sasa kama kuna mwanasiasa analizungumzia jambo hili anatafuta umaarufu tu, kwani lipo katika hatua nzuri na Kamati ya Chisano itatueleza ukweli,” alisema.

Mbio za urais 2015
Wakati huo huo, Rais Kikwete amesema kampeni za kugombea urais kupitia chama hicho, hazijaanza rasmi.
Kutokana na hali hiyo, amesema vitendo vya baadhi ya watu kuanza kampeni kabla ya wakati, ni moja ya mambo yanayosikitisha.
Pamoja na hayo, alisema suala hilo limekabidhiwa kwa Makamu Mwenyekiti wa CCM (Tanzania Bara), Philip Mangula ambaye atalisimamia na kulishughulikia.
Rais Kikwete alitoa kauli hiyo juzi mjini hapa, alipokuwa akizungumza na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mkoa wa Mbeya.
“Kuhusu kama kampeni za kuwania urais zimeanza ni kwamba kampeni hazijaanza rasmi. Hili ni moja ya mambo yanayosikitisha. Lakini suala zima tumelikabidhi kwa Mzee Mangula ambaye atalisimamia na kulishughulikia,” alisema Rais Kikwete.
Rais Kikwete alilizungumzia suala hilo baada ya kuulizwa swali na Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Mbeya, Godfrey Zambi ambaye alimtaka aeleze kama kampeni za urais zimeanza.

MTANZANIA