Miili ya Askari Polisi waliofariki katika ajali ya gari ya kugongana uso kwa uso na basi la Mohamed Trans.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME akiongoza waombolezaji kuaga miili ya Askari Polisi waliofariki katika ajali ya gari.
Waombolezaji.
Miili ya Askari Polisi waliofariki katika ajali ya gari ikiwa imebebwa.
Askari Polisi waliofariki katika ajali ya gari ya kugongana uso kwa uso na basi la Mohamed Trans wameagwa jana Mkoani Dodoma tayari kwa mazishi.
Akiongea kwa masikitiko Kamishna Msaidi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME amewashukuru watu waliojitokeza kuungana pamoja kuaga miili ya Askari hao.
Pia amewataka madereva wote kuwa waangalifu wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto na kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kujitokeza za namna hii.