Mpaka mechi inakwisha ubao wa matangazo ulikuwa unasoma timu ya Yanga 1 na Mbeya City 0
Mshambuliaji machachari wa timu ya Yanga, Mrisho Ngassa (17) akichuana vikali kuwania mpira na beki wa timu ya Mbeya City, Deogratias Julius wakati wa mtanange wa Ligi kuu Tanzania Bara uliomalizika hivi sasa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Dakika 90 za mchezo zimemalizika hivi punde na Yanga imeshinda kwa Bao 1-0 lililotiwa kimiani na Mrisho Ngassa, dakika ya 15 ya mchezo kipindi cha kwanza.
Beki wa Timu ya Mbeya City, Deogratias Julius akijiandaa kuondosha hatari iliyokuwa imekwenda langoni kwao.ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Haroun Niyonzima pamoja na beki wa Mbeya City, Yussuf Abdallah wakiwania mpira, wakati wa mchezo wao wa marudiano katika mzungunguko wa pili wa Ligi kuu Tanzania Bara ulikuwa unachezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mashabiki wa Mbeya City wakiendelea kuishangilia timu yao.
Mbuyu Twite wa Yanga akiangalia nani na kumpatia pasi wakati wa mechi ya Ligi kuu Tanzania Bara.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao lao la kwanza.
Mashabiki wa Yanga wakishangilia timu yao
PICHA NA OTHMAN MICHUZI
PICHA NA OTHMAN MICHUZI