WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, sasa ni wazi ameibua vita nyingine mpya ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), msingi wake ukiwa ni hofu za kuwapo kwa harakati za kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Safari hii, vita hiyo inaonekana kuwa mpya, kutokana na kubeba watu na hoja mpya ambazo ni T-shirt zenye maandishi ya ‘Friends of Lowassa’, zinazodaiwa kuandaliwa na watu wa karibu na Waziri Mkuu huyo wa zamani, pamoja na kauli yake ya ndoto ya kuianza safari, ambayo hata hivyo hajaifafanua hadi sasa.
Kama ilivyokuwa katika vita nyingine, safari hii pia Lowassa anajengewa hoja ya kutimuliwa tena ndani ya chama, sawasawa na ilivyokuwa wakati wa mkakati wa kujivua gamba, ulioshabikiwa sana na wale wanaompinga sasa.
Katika vita hii mpya, katikati yumo Waziri Mkuu wa zamani, ambaye pia ni mmoja wa wanachama wakongwe wa CCM, John Malecela, ambaye ameibuka na hoja hizo, akiungana na makada wengine wa chama hicho, akimtuhumu Lowassa kuwa ndiye anayekivuruga chama, kutokana na kile alichodai kuwa ameanza harakati za kuwania urais kinyume cha taratibu.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Akitumia hoja ya T-shirt kuthibitisha kauli yake, Malecela alidai zinasambazwa na watu wa karibu wa Lowassa kwa minajili ya kampeni za kinyang’anyiro cha kuusaka ukuu wa dola, wakati ambapo kufanya hivyo ni kuvunja kanuni za chama.
Wakati kauli hiyo ya Malecela ikionekana kushtua na kuibua malumbano yenye mjadala mpana, taarifa ambazo gazeti hili limezipata zinaeleza kuwa vigogo wawili ndani ya chama hicho, akiwemo mmoja aliyepata kushika wadhifa mkubwa serikalini, nao wameapa kujitokeza hadharani kumuunga mkono Malecela, endapo wataona kauli yake imepuuzwa.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula, naye ameiunga mkono kauli hiyo ya Malecela, hatua ambayo imeibua hisia za kuwapo kwa mpasuko mkubwa ndani ya chama hicho.
Kauli ya Malecela na Mangula ambazo zote zimetolewa ndani kipindi cha wiki moja, ikitanguliwa na ile iliyotolewa na mmoja wa viongozi kutoka katika kundi la Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM), Paul Makonda, imewafanya baadhi ya wasomi na watu wa kada mbalimbali waone hatari inayoikabili CCM mbele.
Ingawa Lowassa mwenyewe hajawahi kutamka bayana kuwa atawania urais mwaka 2015 na amekataa kujibu tuhuma zinazoelekezwa kwake na hata alipotafutwa tena jana na gazeti hili kupitia simu yake ya mkononi ambayo iliita bila kupokelewa, anaonekana kuibua vita hii mpya, msingi wake unaaminika kuwa ni kauli aliyoitoa wakati wa sherehe za kuukaribisha mwaka mpya wa 2014, nyumbani kwake, Monduli.
Katika sherehe hizo, Lowassa alitangaza kuwa ana ndoto ya kuanza safari ambayo hakuifafanua, lakini aliita kuwa ni ya matumaini na kwamba atafika kwa nguvu za Mungu.
Wakati mapambano haya yakitokea, sasa wana CCM, wakiongozwa na Mwenyekiti wao wa Taifa, Rais Jakaya Kikwete, leo wanatarajia kuadhimisha sherehe za miaka 37 ya chama hicho, huku malumbano hayo yakitajwa kuzidi kukiacha chama katika mgawanyiko mkubwa.
Tayari Rais Kikwete ameshauriwa na baadhi ya watu wa kada mbalimbali, wakiwemo wasomi, kutafuta suluhu mapema kutokana na kile ambacho kimejitokeza ndani ya wiki hii, ili kukinusuru chama na mgawanyiko ambao unaweza kuleta mpasuko mkubwa ambao utakifikisha 2015 kikiwa vipande vipande.
Profesa Mwesiga Baregu, Dk. Benson Bana pamoja na wasomi wengine wa sayansi ya siasa, kwa nyakati tofauti wamekaririwa na vyombo vya habari wakitahadharisha mwenendo huo wa malumbano ndani ya CCM na kushauri kutafutwa kwa vikao rasmi kuweza kuyaondoa ili kulinda afya ya chama.
Ingawa baadhi ya wachambuzi na wafuatiliaji wa siasa za chama hicho wanasema kuwa CCM haijawahi kuwa moja kwa miongo na miongo, lakini kusambaratika huko kunaelezwa kuja kwa sura tofauti tofauti ambazo zimekuwa zikiacha alama mbaya kwa chama.
Sura hizo ni pamoja na kuchomoza kwa makundi ya watu wanaousaka urais nyakati ambazo Uchaguzi Mkuu unakaribia, hali ambayo wakati mwingine imekuwa ikiacha alama za vidonda na hivyo kusababisha visasi baina ya wanachama.
Nyingine ni vikumbo vinavyotokana na baadhi ya makada wake kuenguliwa kugombea nafasi za uongozi, kutofautiana misimamo katika jambo fulani, lakini kwa misingi hiyo hiyo ya kimakundi.
Wakati Lowassa akionekana kulengwa zaidi katika vita hii, lakini yapo makundi mengine ndani ya chama hicho ambayo nayo yanatajwa kuanza harakati zake, lakini yamekuwa hayaguswi kwa namna kama anayoguswa Mbunge huyo wa Monduli.
Baadhi ya makada wa CCM wanaotajwa kuwania nafasi ya ukuu wa dola katika uchaguzi wa mwakani, mbali na Lowassa, wengine ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Uhusiano, Steven Wassira, Rais wa Zanzibar, Dk Mohamed Shein.
Wengine ni aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja na Waziri wa Mambo ya Ndani, Emanuel Nchimbi, ambaye hata hivyo baadhi wanasema kuwa huenda harakati zake zikawa zimedhoofishwa kutokana na hatua ya Rais kumvua madaraka.
Kwenye kundi hili pia yumo Naibu Waziri wa Mawasiliano, January Makamba, Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli na wengine.
MGEJA AIBUKA AMRARUA MALECELA
Ni katika mwendelezo huo wa malumbano ya sasa, jana Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja, aliitisha mkutano na waandishi wa habari, Jijini Dar es Salaam na kumshangaa Malecela kwa kutoa kauli ambazo mbali na kutokuwa na uthibitisho, lakini zisizopaswa kutolewa na mtu mwenye heshima zake kama yeye.
Mgeja alisema Malecela alipaswa kuwa mtu wa kwanza kumuongoza kijana Makonda katika njia sahihi, lakini badala yake, naye amepotoka na kuonekana kama mtu aliyefilisika kifikra kutokana na kutoa matamshi yenye vijembe ambayo hayana tija kwa maendeleo ya Taifa.
Alimkumbusha Malecela jinsi hata yeye alivyowahi kutuhumiwa huko nyuma kuwa alipewa fedha kutoka nchi za Kiarabu, hali iliyomfanya abadili dini na jina na kuitwa Jumanne, ili aungwe mkono kupewa nguvu za kugombea urais.
Kuhusu uchu wa urais anaotuhumiwa Lowassa, Mgeja alisema Malecela amesahau kuwa yeye ndiye ana uchu mkubwa wa madaraka, kwani amepata kuomba nafasi ya urais mara kadhaa huko nyuma, lakini hakupata nafasi hiyo kwa sababu hatoshi.
Alidai kuwa uchu huo wa madaraka wa Malecela ndio uliomsukuma hayati Mwalimu Nyerere kutunga kitabu cha ‘Uongozi wetu na hatima ya Tanzania’ na kwamba hiyo ilikuwa ni kuonyesha kuwa Malecela alikuwa sugu wa matatizo yanayokiuka maadili.
“Jambo lingine ni kwamba Mzee Malecela ameshindwa kutambua kuwa wanaokivuruga chama ni wale wanaozungumza nje ya vikao halali vya chama na jumuiya zake…lakini Mzee Malecela na Makonda na washirika wenzao wanajua kinachoendelea nchini, wako baadhi ya wanachama wanagawa kalenda na simu nchi nzima, huku wakitumia magari ya serikali na inawezakana na wao walikwishazipokea na hata mimi niliishazipokea, mbona hizo hawasemi nazo zinakivuruga chama?” alihoji Mgeja
Mgeja alisema kama nchi imefika pabaya, kwani kila mmoja amebaki kuwa mlalamikaji na kutuhumiana pasipokuwa na ushahidi, jambo alilosema kuwa ni hatari kwa mustakabali wa Taifa.
Katika hilo pia alitahadharisha watu kumgeuza Lowassa kuwa ajenda ya kitaifa, huku wakiacha mambo muhimu yanayoigusa nchi na maisha ya Watanzania kwa ujumla.
Akimzungumzia Makonda, alisema kauli yake ya kuwatuhumu baadhi ya viongozi wa dini pamoja na vijana kuwa kama wanataka fedha za bure waende kwa Lowassa ni kuwavunjia heshima viongozi hao.
Alisema anaamini kuwa kuna genge la wahafidhina lililoko nyuma yake ambalo linamtumia na kumtaka Mwenyekiti wa Vijana wa Taifa athibitishe iwapo kauli hiyo ni ya Umoja huo ama ni binafsi.
Wakati Mgeja akisema hayo, ikumbukwe kuwa msingi wa malumbano ya sasa ni kauli iliyotolewa zaidi ya wiki moja iliyopita na Mwenyekiti mstaafu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita, ambaye aliwataka viongozi wa sekretarieti ya CCM, ambao ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, kuacha kuingilia uteuzi wa Baraza la Mawaziri uliofanywa na Rais Kikwete hivi karibuni.
Ni kauli hiyo ndiyo iliyomuibua Makonda, ambaye alidai kuwa wapo watu wanaofadhiliwa na Lowassa ili kuwashambulia viongozi wa sekretarieti ya CCM, kwa kuwa anautaka urais mwakani na kutamka bayana kuwa amekosa sifa za kuteuliwa na chama kuwania wadhifa huo.

MTANZANIA