Mi nimetoka mtaa wa pili hapo nshazinguana na mademu flani walikuwa wanataka kuniletea za fesibuku nikawashtukia, nikawachana, wamemaindi nikaona isiwe tabu, nikaachana na kibaa chao ikabidi nije maskani tupige stori.
… Inakuwaje kwanza?
Uko fresh?
Us’konde wala nini mwanangu, naona kama nataka kukuzingua vile, mi leo amani tu hapa, na sikuulizi mambo ya mwaka unaoisha najua ulizingua watu sana mwaka huu, acha uende tugange yajayo.
Uongo?
Najua unaitaka hii stori ya mademu niliozinguana nao mwanangu, ntakupa ila kwanza ngoja niwarushe wanangu wanaonisoma deile ambao mwaka umeisha huku wakiendelea kunipiga tafu, kwa kulifuatilia Zee kila linakokatiza.
ENDELEA KUSOMA STORI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
ENDELEA KUSOMA STORI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Mwanangu Eddy Seng wa Mabegi bila nauli, Fisi, Rioba, Makunga, hata wewe pia mwanangu Big Up, mwaka ushasepa, tugange yajayo.
Sasa hao mademu bwana mi siyo kwamba walikuwa washkaji zangu wala nini, walikuwa ni watu tuliokutana nao fesbuku humu, kila siku wananizingua mara Ooh, ..Zee ibuka kiwanjani kwetu tule gambe na nini ... Mi nikawa nawakata stimu tu kwa kuwapigia stori za waifu.
...Si unajua zile...
Unafkiri wanakoma sasa, wakawa kama wanakomaa tu hivi kwa kuweka picha zao za kujiseksisha, mara tutoke nini, sasa kila nikiwaangalia nikawa kama nazimika hivi, watoto wakali kweli ujue?
Siku moja mtu mzima nikaona kwani nini? Siyo kesi, ngoja nikajimiksi na watoto wazuri na mimi nioshe vumbi, ingawa kiukweli mtoto mkali kuliko wote ni waifu wangu na ndiyo maana yuko homu pale.
..ukiona vipi pigana...
Ila kilichokuwa kinanizingua kwa wale mademu unajua kilikuwa nini, mara wako bichi, kesho wako kwenye hoteli kubwa wanakula bata, mara keshokutwa unakuta statasi mtu yuko JK Eapoti anasepa, nikaona watoto hawa siyo wale wa kutiana mawazo watakuwa fresh ngoja wawe washkaji.
Maana kuna wale uswazi taipu ambaye dakika chache baada ya kujuana simu inaisha krediti, mara itaibiwa, na keshokutwa ataibiwa waleti na hela zote kaweka humo, mwisho mtu mzima unaanza kuona ya kazi gani sasa, unasepa.
Sasa hawa walikuwa wamejipanga, siku ya kwanza nikawaibukia, mwanangu kwanza sura zao na zile za kwenye fesibuku ...tofauti mwanangu, kidogo nitoke nduki ila nikajipa moyo kwamba si wana, kwani wachumba, kwenye wana hata wangekuwa magorila ingekuwa fresh tu.
Haya ikaja zamu ya gambe na kulipa bili, kila kikiletwa kikaratasi unakuta wote wameomba ekschuzi wameenda toileti, halafu zile gambe nilizokuwa naziona kwenye picha mbona kama hazifanani nao? Kwani niliwakopesha? siku inayofuata nikaachana nikawaambia wanangu hizi laifu feki za fesibuku zinawapoteza, kama vipi jipangeni kuna mengi mapya na mazuri ya kufanya.
...Mnapotea!
Mwaka unakuja huu haina haja ya kujifeki, ukijifeki ndiyo unafeki maisha yako na maisha yako yakiwa feki unafikiri kuna nini tena mwanangu mwenyewe?
Mi nach’kua taim...
MWANANCHI