MAREHEMU SELINA MAKINGI (MAMA ADAM)
Serikali ya Wanafunzi Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Kampasi ya Dodoma (COBESO) Imepokea taarifa za kifo cha Mfanyakazi wa Chuo Marehemu Selina Makingi (Mama Adamu) kwa masikitiko makubwa.
Kwa niaba ya Wanafunzi wote Rais wa Serikali ya Wanafunzi CBE - Dodoma Mh. Remidius M. Emmanuel anatoa pole kwa Wafanyakazi wote wa Chuo cha CBE pamoja na ndugu jamaa na Marafiki waliofikwa na Msiba huo.
Taarifa za Msiba huu zimeifikia Serikali ya COBESO Mapema Asubuhi ya Leo (27/12/2013) kutoka kwa Kaimu Afisa Mwandamizi Rasilimali watu na Utawala Bi. Msemo, N . Ambaye kupitia taarifa yake amesema Bi. Selina Makingi Amefariki leo Asubuhi Desemba 27, 2013 katika Hospitali ya Mkoa Dodoma, na kuongeza kuwa Taratibu nyingine za msiba zitaendelea kutolewa.
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA.
JINA LA BWANA LIHIMIDIWE
AMINA.