Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

MEMBE: SITAGOMBEA UBUNGE 2015 NA PIA AITAKA CCM IJISAFISHE KUELEKEA UCHAGUZI 2015

$
0
0
 
Waziri Membe wakati akizungumza katika kipindi cha Dk. 45 cha ITV.amesema  kuwa hatagombea ubunge 2015 ni baada ya Mtangazaji wa ITV, Emanuel aliuliza swali kwamba kajipangaje na uchaguzi 2015 yeye amesema hatagombea ubunge lakini kagoma kusema atagombea kakataa kusema atagombea Urais, Anasema ameshaombwa sana na watu wengi kwamba agombee. Na pia kasema CCM lazima ijisafishe au wakisafishe ili washinde uchaguzi na pia amesema chama lazima kiangalie utajiri wa wanachama wake na kwamba wameupata wapi hapa ni kama anasemwa Lowassa

Pia alizungumzia  mgogoro wa Sudani Kusin anasema mpaka sasa watu kama 500 wameshapoteza maisha anasema kuna watu wengi wako katika eneo la mapiganolakini  wako salama, Amesema watanzania walioko Sudan Kusini waende wakajiandikishe kwenye ubalozi wa Kenya ili wafanye utaratibu wa kuwaondoa kwani hali ni mbaya mpaka sasa

ENDELEA KUSOMA HABARI  HIII KWA KUBOFYA HAPA CHINI 


Adai mgogoro unaoendelea CHADEMA ni harakati za kisiasa, Waziri wa mambo ya nchi za nje Bernard Membe amesema waraka ulio mhukumu Zito hauna shida yoyote. Wanamuonea tu kijana yule. Amesema vurugu alizofanya, mgawanyiko anaoleta katika CHADEMA ni harakati halali za kidemokrasia.
Pia katika maelezo yake katika kipindi cha dakika 45 kiachorushwa na ITV kwasasa inaonyesha amejiandaa kugombea urais kwani amesema hagombei ubunge tena. Alipobanwa zaidi namwandishi akasema ingawa hajaoteshwa wanachama wa CCM ndio watakaoamua

Waziri wa mambo ya nchi za nje Bernard Membe amesema anaitaka CCM ijisafishe kuelekea uchaguzi mkuu 2015. Akiongea katika kipindi cha dakika 45 amekiri CCM lazima kijisafishe chenyewe, na kuhakikisha ifikapo 2015 chama kipo safi na imara.

Waziri Membe amesema maneno ambayo ni nadra sana kusemwa na viongozi wa CCM, pale aliposema hatupo tayari tuingie kwenye uchaguzi kukiwa na uchafu, na ni heri tubaki wachache tushindwe uchaguzi kuliko kufanya kosa la kuwakumbatia wachafu eti kisa tunataka kushinda.


Membe amemwambia mwandishi kuwa akumbuke 2015 tunakwenda kushindana na CHADEMA, hivyo chama chake lazima kijiandae vyema.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>