Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Rais wa Afrika kusini Jacob Zuma akilihutubia taifa kupitia bunge la nchini humo
Bunge la Afrika kusini liligeuka kuwa uwanja wa vita ambapo wabunge wa upinzani ilifikia hatua ya kuvutana mashati na maafisa wa usalama na kufanya wabunge wa upinzani wa chama cha Economic Freedom Fighters (EFF) wakiongozwa na Julias Malema kutolewa nje ya ukumbi wa bunge kwa nguvu na baadae wabunge wengine wa upanzani nao wakatoka nje ya ukumbi.
Wabunge wa upinzani wa chama cha Economic Freedom Fighters (EFF) wakiongozwa na Julias Malema wakitolewa nje ya ukumbi wa bunge kwa nguvu na maafisa usalama wa nchini humo.
ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Sakata hilo lilizuka wakati Rais wa nchi hio Jacob Zuma alipokuwa akilihutubia taifa na kuulizwa maswali na wabunge wa chama cha EFF kinachoongozwa na Julius Malema wakitaka kujua ni lini atarejesha pesa zilizojengea jumba lake la kifahari la Nkandla
Wabunge wengine wakitoka bungeni baada ya kutokea vurugu kwenye bunge la nchini Afika Kusini(Picha na Yahoo)