Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Moto uliozuka mapema leo katika nyumba moja iliyopo kati ya mtaa wa Jamhuri na Mosque jijini Dar es Salaam na kuteketeza mali kadhaa ambazo bado haijaulikana thamani yake na kutokana na mashuhuda waliokuwepo wakati moto huo ukianza kuwaka wanafikiri moto huo huenda umesababishwa na hitilafu ya umeme lakini msemaji kutoka kikosi cha zima moto amesema chanzo kamili cha moto huo bado hakijajulikana.
Kikosi cha zimamoto na Jeshi la Polisi wakiwa eneo la tukio. Picha zote kwa hisani ya Othman Michuzi
Gari la Zimamoto la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Dar es Salaam likiwasili eneo la tukio.
Kazi ikiendelea.
Mamia ya wakazi wa Jiji la Dar wakishuhudia tukio la Moto Mkubwa uliozuka mapema leo kwenye majengo matatu ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) yaliopo kwenye makutano ya mtaa wa Libya na Mosque kuteketeza eneo lote la juu la Majengo hayo.Chanzo cha moto huo hakikuweza fahamika mpaka tunaingia mitamboni japo tetesi zinaeneleza kwamba ni hitilafu ya umeme.
Mwanalibeneke Othman Michuzi (kushoto) akiwa katika mavazi maalum pamoja na Maafisa wa Kikosi Zimamoto wakati wa zoezi la uzimaji moto huo mchana wa leo jijini Dar.
Sasa tumemaliza kazi na shukrani za dhati kwa maafisa wa kikosi cha Zimamoto waliokuwa bega kwa bega na wanahabari kuhakikisha uzimaji wa moto huo unakwenda vema.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalim ya Dar es Salaam,Kamishna Suleiman Kova akizungumza na vyombo vya habari.
Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Jeswad Nkongo akizungumza na vyombo vya habari juu ya walivyofanikiwa kuudhibiti moto huo.