Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limesema usahihishaji wa mitihani ya kidato cha nne uliofanyika Novemba mwaka jana, umekamilika. Hatua hiyo inafuatia baadhi ya wanafunzi waliomaliza kidato cha nne kuwa na shauku ya kutaka kufahamu walichovuna kutokana na kukaa darasani kwa miaka takribani minne.
Kwa mujibu wa Katibu mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde amesema kuwa usahihishaji umekamilika na baraza lipo katika uchambuzi wa kuyapanga na yatakapokamilishwa watayatangaza.
Aidha, Katika kipindi cha miaka miwili mfululizo, mwaka 2012 na 2013, Necta ilitangaza matokeo ya kidato cha nne mwishoni mwa Februari na mwanzoni mwa Machi.
Katika hatua niyinge muhula wa masomo kwa kidato cha tano huanza Julai, huku mwezi Machi na Aprili mchakato wa kuwapangia shule hufanyika wakati Mei na Juni hutumiwa kwa maandalizi ya kuripoti shule wanafunzi waliofaulu mtihani huo.
CHANZO: TIMES FM