Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Meneja wa kitengo cha maafa wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Abubakari Ndwata(wa tatu kutoka kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, Mwaija Lipinga(wa pili kutoka kushoto) msaada wa mabati 92 yenye thamani ya 2 mil. kwa ajili ya kuezekekea Bweni la wasichana wa shule ya Sekondari Mpwapwa baada ya lililokuwepo kuungungua na moto hivi karibuni.
Mkuu wa shule ya Sekondari Mpwapwa Nelson Milanzi akisoma taarifa mbele ya maofisa toka Mfuko wa Pensheni wa LAPF kuhusu Bweni la wasichana 84 wa shule ya sekondari Mpwapwa lilivyoungua na namna wadau mbalimbali wanavyoendelea kutoa misaada ambapo Mfuko wa Pensheni wa LAPF walitoa baadhi ya misaada shuleni hapo.
Maofisa wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF wakiongozana na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa pamoja na Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa walipoitembelea Shule ya Sekondari ya Mpwapwa na kujionea namna bweni hilo lilivyoongua na moto hivi karibuni kabla ya kutoa msaada wa Mabati 92 kwa ajili ya kuezekea jengo litakalojengwa.
Viongozi hao wakiangalia mabaki ya wanafunzi wa kike wa Shule ya sekondari mpwapwa yaliyozagaa baada ya Bweni lao kuungua na moto hivi karibuni.
Wageni mbalimbali wakiangalia jengo hilo lilivyoungua kwa ndani
Huu ndo muonekano wa ndani pamoja na nje ya bweni lililoungua kwa moto