Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasilina anasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Nahodha wa Ivory Coast, Yaya Toure akipokea kombe la ubingwa wa Mataifa ya Afrika (AFCON 2015 ) baada ya kuifunga Ghana kwa mikwaju ya penati na kutangazwa kuwa mabingwa wapya wa michuano hiyo.
Ivory Coast ndio mabingwa wa fainali za mataifa Afrika zilizofikia kilele chake hapo jana nchini Equatorial Guinea baada ya kuifunga Ghana katika mikwaju ya penati.
Katika mchezo huo wa fainali, timu hizo zilijikuta zikimaliza dakika 90 zikiwa hazijafungana, na hata katika muda wa nyongeza wa dakika 30 pia zilishindwa kufungana.
Ndipo mikwaju ya penati ilipotumika kupata mshindi, ambapo Ivory Coast walipata penati 9 dhidi ya 8 za Ghana.