Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (kushoto) akipeana mkono Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alipotembelea ofisi za gazeti la Tanzania Daima.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnuye akikutana na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alipofika katika Ofisi za Free Media, wachapishaji wa gazeti la Tanzania Daima, akiwa katika ziara katika vyombo vya habari ambayo aliianza juzi, jijini Dar es Salaam.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana kwa furaha na Mhariri Mtendaji wa Free Media, Nevile Meena alipowasili kwenye kampuni hiyo leo akiwa katika ziara kwenye vyombo vya habari mjini Dar es Salaam
Nape akizungumza na baadhi ya viongozi wa kampuni ya Free Media wachapishaji wa gazeti la Tanzania Daima leo jijini Dar es Salaam
Nape akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika Ofisi za gazeti la Jambo Leo, leo mjini Dar es Salaam, akiwa katika ziara hiyo. Wapili kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Concept inayochapisha gazeti hilo, Teophil Makunga.
Nape akiwa katika mazungumzo na uongozi wa kampuni ya Jambo Concept
Nape akifafanua jambo wakati wa mazungumzo hayo na uongozi wa Jambo Concept
Nape akimuonyesha Makunga Kalenda ya CCM ya mwaka huu (2015) kabla ya kumkabidhi kama zawadi.
Nape akimkabidhi zawadi ya kalenda ya CCM, Makunga
Baadhi ya waandishi wa habari katika chumba cha habari cha magazeti ya Jambo Leo
Nape akiwa kwenye chumba cha Breaking news cha magazeti ya Jambo Leo
Nape akiagana na mpigapicha mkuu wa Jambo Leo Richard Mwaikenda mwishoni mwa ziara katika chumba cha habari cha magazeti hayo. Picha na Bashir Nkoromo na Adam Mzee