Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

VURUGU KUBWA ZATOKEA KWENYE MECHI YA NUSU FAINALI KOMBE LA AFCON 2015 KAYI YA GHANA NA EQUATORIAL GUINEA

$
0
0
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.

  
 Askari polisi wakiwa wamewazingira wachezaji wa timu ya taifa ya Ghana kuwapa ulinzi kufuatia vurugu kubwa zilizoibuka uwanjani baada ya mashabiki wa Equatorial Guinea kurusha vitu mbalimbali uwanjani baada ya timu yao kutandikwa mabao 3-0.
Helkopta ikiimarisha ulinzi uwanjani hapo kufuatia vurugu zilizoibuka katika mchezo huo

ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Chupa za maji zikirushwa uwanjani huku askari polisi wakiwa wamejipanga kuwalinda wachezaji wa timu ya taifa ya Equatorial Guinea.


Timu ya soka ya taifa ya Ghana " Tha Black Stars " wamefuzu kucheza mchezo wa fainali wa kuwania kombe la mataifa ya Afrika baada ya kuwatandika wenyeji wa michuano hiyo, Equatorial Guinea kwa mabao 3-0 katika mchezo wa nusu fainali uliochezwa usiku wa kuamkia leo. 
Hata hivyo mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Malabo, ulishuhudia kuibuka kwa vurugu kubwa uwanjani hapo zilizosababishwa na mashabiki wa Equatorial Guinea walioanza kurusha chupa za maji uwanjani na kuwafanya polisi kuingia kazini. 
Katika mchezo huo, mabao ya Ghana yalifungwa na Jordan Ayew katika dakika ya 42 kwa mkwaju wa penati. Bao la pili lilifungwa na Wakaso katika dakika ya 45 na bao la tatu likawekwa kimiani na Andrew Ayew katika dakika ya 75. 
Kwa matokeo hayo, Ghana sasa inakutana na Ivory Coast katika mchezo wa fainali siku ya jumapili.
 Furaha ya ushindi, wachezaji wa Ghana wakifurahia kufuzu kucheza fainali ya michuano ya Afcon 2015


Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>